Rasmi Ibrahim Ajib Migomba atia saini kuitumikia yanga miaka 2

Rasmi Ibrahim Ajib Migomba atia saini kuitumikia yanga miaka 2

View attachment 536093

Dar es Salaam. Baada ya kuwepo kwa tetesi za muda mrefu, straika Ibrahim Ajib amesaini rasmi mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga ambayo ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu.

Ajibu amesaini mkataba huo leo mbele ya mabosi wa Yanga na kutambulishwa rasmi kwa mashabiki wa klabu hiyo.

Nyota huyo anakuwa mchezaji wa pili kusainiwa na Yanga katika usajili wa sasa huku klabu hiyo ikiwa mbioni kukamilisha usajili wa kiungo wa Mbeya City, Raphael Daudi
Ibrahim Ajib asaini rasmi klabu ya Yanga

Yanga inaongozwa kizee sana, viongozi waliopo hawaenda na mfumo wa soka la kisasa..

Tazama Azam, Mbeya Situ, Singida United na Simba wanavyowatambulisha wachezaji wao, mdhamini anapata mileage kutokana na brand zinazofanyika, Singida United ya juzi tu lakini press zao kuna banner za wadhamini wao puma, nmb, sportpesa, orxy.

Yanga viongozi wanawaza kuuza sura tu kwenye camera, mchezaji anasaini mkataba mbele ya viongozi sita wote wana kazi gani?

Hatuoni vilabu vingine vinavyofanya? Mkataba wanasaini watu wawili ila kuna jaa watu kibao kuuza sura tu, huu ni ushamba.

Yanga inadilike, kama mdhamini sportpesa anayetoa mil 950 kwa mwaka unahsindwa kumtanbaza, unategemea utapata wapi wadhamini wengine?
 
Si habari njema kwa upande wa pili...
Aliondoka Ronaldo pale man u sembuse ajibu, kwani nyinyi mlitaka akitoka simba aende WAP? Ile ni kazi yake yuko tayar kufanya kaz na club yoyte na cyo yanga na simba tu, hebu mashabiki tufike mahala na sis tuwe waelewa kidogo basi, Simba nguvu moja.
 
August 19 mechi na mikia..1)Youthe Rostand2)Abdul 3)Mwinyi 4)Yondani 5)Canavaro 6)Moyo 7)Raphael Alpha 8)Kamusoko 9)Tambwe 10)Ngoma 11)Ajibu au Chirwa.....Mnyamaaa kajipangeee
 
August 19 mechi na mikia..1)Youthe Rostand2)Abdul 3)Mwinyi 4)Yondani 5)Canavaro 6)Moyo 7)Raphael Alpha 8)Kamusoko 9)Tambwe 10)Ngoma 11)Ajibu au Chirwa.....Mnyamaaa kajipangeee
Y chirwa mnamsahau Hv?
 
Hata hivyo ajibu hayuko vizuri kisaikolojia ..
Yaani kijana Simba Sports, imemlea imemkuza anafikia kilele cha mafanikio anahamia timu pinzami ili awafunge walezi wake..!
Ni bora Simba Sports imeachana na kulea vijana wa mpira.
Unamlea mtu vizuri kumbe anamapenzi na mhasimu wako wa mpira.
Amog alikuwa sahihi kumuweka benchi kwenye baadhi ya mechi.
Tunamtakia mafanikio mema huko anakoenda madhani atafurahia kufanya kazi kwenye timu anayoipenda.
 
August 19 mechi na mikia..1)Youthe Rostand2)Abdul 3)Mwinyi 4)Yondani 5)Canavaro 6)Moyo 7)Raphael Alpha 8)Kamusoko 9)Tambwe 10)Ngoma 11)Ajibu au Chirwa.....Mnyamaaa kajipangeee
Hivi mmewahi kushinda hata match 1 tu tangu unaandika comment hii
 
Back
Top Bottom