Rasmi: Kocha Pitso Mosimane asaini mkataba mpya wa miaka miwili Al Ahly

Rasmi: Kocha Pitso Mosimane asaini mkataba mpya wa miaka miwili Al Ahly

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Kocha Mkuu wa Klabu ya Al Ahly ya Misri, Pitso Mosimane (57) raia wa Afrika Kusini ameongeza mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kuitumikia timu hiyo hadi msimu wa mwaka 2023/24.

Mosimane alitangazwa rasmi kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo Oktoba mwaka 2020 akitokea ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Taarifa hii imethibitishwa na Al Ahly wenyewe ambao kupitia kurasa zao za kijamii na tovuti wametangaza juu ya mkataba huo mpya ambapo pia wasaidizi wa kocha huyo nao wameongeza mkataba wa miaka miwili.

Awali ilikuwa ikiaminika kocha huyo atafukuzwa au kuondoka klabuni hapo baada ya mkataba wake kuwa unaelekea ukingoni, wakongwe kadhaa wa Al Ahly waliowahi kucheza kikosini hapo na wachambuzi wa Misri walikuwa wakimshutumu kuwa hana uwezo wa kuifundisha timu hiyo.

128566476_2763202860559601_1875861952980794034_o.jpg
 
Kuna watu husema waarabu ni wabaguzi. Huyu amepiga kazi kweli kweli lakini bado anasemwasemwa labda wanaosemaga wana ukweli.
 
Kuna watu husema waarabu ni wabaguzi. Huyu amepiga kazi kweli kweli lakini bado anasemwasemwa labda wanaosemaga wana ukweli.
Ni dhana imejengwa kwa muda mrefu..Ni kama kusema Waarabu walikuwa wakiuza watumwa.
 
Wenzetu wanatangaza nchi zao,from SA to Egypt...kwetu ni from kahama to kibondo...
 
Naangalia game ya al ahly na mamelody, aisee al ahly mpaka dakika hii hawajapata goli!!!

Hapo hakuna kocha,, wamepigwa. Al ahly co ile tunayoijua ilikua inapiga mtu goli 5.
 
Naangalia game ya al ahly na mamelody, aisee al ahly mpaka dakika hii hawajapata goli!!!

Hapo hakuna kocha,, wamepigwa. Al ahly co ile tunayoijua ilikua inapiga mtu goli 5.
Wameshatanguliwa goli moja. Kama matokeo yatabaki hivi basi Mamelod watakuwa wameshajikatia tiketi ya hatua inayofuata. Al Ahly itabidi kupambana na wasudan kugombania nafasi ya pili
 
Wameshatanguliwa goli moja. Kama matokeo yatabaki hivi basi Mamelod watakuwa wameshajikatia tiketi ya hatua inayofuata. Al Ahly itabidi kupambana na wasudan kugombania nafasi ya pili

Yah nimecheki. Mamelody 35% al ahly 65%
 
Yah nimecheki. Mamelody 35% al ahly 65%
Hiyo possession haitoi picture ya kilichokuwa kinatokea uwanjani. Ahly walipigiwa mpira ila mbaya.ile mechi ya kule Misri,Sundown walizidiwa sana
 
Hiyo possession haitoi picture ya kilichokuwa kinatokea uwanjani. Ahly walipigiwa mpira ila mbaya.ile mechi ya kule Misri,Sundown walizidiwa sana

Hata hii walizidiwa sana mamelody, sema ahaly bahati haikuwa yao. All in all ushindi ndiyo kila kitu.
 
Back
Top Bottom