RASMI: Kocha wa Azam FC, Youssouph Dabo avunjiwa mkataba

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
1725357015161.png
Azam FC imetangaza leo, Septemba 3, 2024, kwamba imefikia makubaliano ya pande mbili na kocha mkuu Youssouph Dabo ya kusitisha mahusiano yao ya kikazi. Dabo, ambaye amehudumu katika klabu kwa kipindi cha mwaka mmoja, anaondoka pamoja na wasaidizi wake wote wa benchi la ufundi aliokuja nao.

Soma Pia: Kocha wa Azam keshapewa thank you

1725357178355.png
 
Klabu ya Azam Imemufuta Kocha Wake Yusuphu Dabo Kufuatia Matokeo Mabaya Ambayo Imeyapata hivi Karibuni Katika Mashindano Ya Klabu Bingwa .

1725357184053.jpg

Uamuzi Huo Unaendana Na Kulifuta Benchi Zima La Ufundi Ambalo Lilikuwa Linafanya kazi Na Mwalimu Yusuphu Dabo pamoja Na Wasaidizi Wake.

Taarifa Inaonyesha Kuwa Timu Ya Azam Itakuwa Chini ya Kocha Wa Vijana Pindi Ambapo Uongozi utakuwa unatafuta Kocha Mpya
Chanzo Via Azam fc
 
watuletee mwengine nae tumlambe goli tano hata kumuaga wasimuage kabisa!
 
Kwa Azam tatizo linaanzia kwenye management

Yusuph Bakhressa siku atayoamua ku fire management ya wazawa na kuweka watu wa mpira kutoka mataifa mengine nadhani kuna changes ataziona.

Sababu ya kufanya hivyo inatokana na kwamba watanzania wote tuna interest na vilabu viwili tu.

Sasa inapokuja suala zima la uongozi kwenye hizi timu zingine ukaweka wazawa maana yake ipo nafasi kubwa ya wao kusukumwa na mahaba ya hizo Club na kwenda kuihujumu timu ambayo imewaajiri.
 
Menejimenti ya azam ni wadogo zake watano wa damu na baba yake mdogo

Atawafukuzaje mkuu?
 
Hilo nalo lina changamoto yake. Matajiri wetu wamezowea kufanya kazi na walio watiifu kwao hata kama ni kinyume na alumna, Sheria na maadili. Kwa hivyo benchi la kutoka nje ya nchi siyo hoja, hoja ni iwapo litaweza kusimamia lililo sahihi kwao na kwa taaluma yao, au litafuata matakwa ya tajiri ilimradi tu mkono wende kinywani.
 
Mi sijazungumzia eneo dogo la benchi la ufundi.

Benchi la ufundi ni sehemu ndogo sana na hii mbona ni kawaida kuona foreigners wakipewa nafasi eneo hilo.

Mii nazungumzia mfumo wa uendeshaji timu katika ngazi ya kimadaraka wawekwe watu ambao hawana mahaba na timu yeyote ya hapa Bongo.

Awe ni mwajiriwa wa nje mwenye taaluma yake ambaye kakabidhiwa majukumu ya kiuongozi.
 
Menejimenti ya azam ni wadogo zake watano wa damu na baba yake mdogo

Atawafukuzaje mkuu?
Kauli ya Dube haikuwa uongo ujue.

Hapo sasa atachagua mwenyewe aiache timu ijiendeshe kwa namna mbovu ya viongozi kufurahia kupoteza mechi dhidi ya Simba au Yanga ili kulinda undugu.

Au akubadili mabadiliko ya kuwaweka watu wasiokuwa na upande ili wao wasimame kama waajiriwa wa hiyo Club afikie malengo.
 
Hapo azam tatizo ni kaka yao mkubwa yule ndio tatizo mbaya zaidi yeye ndio boss yule mtoto wa bakhresa
 
Kwa Azam tatizo linaanzia kwenye management

Yusuph Bakhressa siku atayoamua ku fire management ya wazawa na kuweka watu wa mpira kutoka mataifa mengine nadhani kuna changes ataziona.

Sababu ya kufanya hivyo inatokana na kwamba watanzania wote tuna interest na vilabu viwili tu.

Sasa inapokuja suala zima la uongozi kwenye hizi timu zingine ukaweka wazawa maana yake ipo nafasi kubwa ya wao kusukumwa na mahaba ya hizo Club na kwenda kuihujumu timu ambayo imewaajiri.
Mahaba vs 5M mshahara?
 
Ni sahihi. Refer kile Dube alichokiongea.
 
Wajinga tuu ndio wanamahaba na vilabu hivyo viwili baada ya mpunga.
 
Tatizo la Azam si kocha, watafukuza kila kocha, shida ya Azam ni wachezaji bado timu haina mbadala sahihi wa Dube na Kipre Junior. Pia viungo wakabaji Akaminko bwana rafu hana mbinu ingine kukaba na Mtasingwa bingwa wa kuzurura tu uwanjani, hawa hawana ubora wa kucheza Azam.
Azam wasajili tena sehemu hizo nilizotaja matokeo watayaona.

Sijui mwanangu anaipendea nini hii timu wachezaji hawajitumi kabisa sababu hawagombanii namba.
 
Back
Top Bottom