TODAYS
JF-Expert Member
- Apr 30, 2014
- 14,747
- 24,250
Tulikuwa tumekaa sehemu tunatafakari safari yetu ya maisha kwa hizi piga nikupige za hapa na pale, baadaye tunasoma breaking story ya kifo cha camaraderie Bernard Camirius Membe.
Binafsi nilienda moja kwa moja kwenye kumbukukumbu za kampeni za urais mwaka ule ambao marehemu aliondoka kwa gafla kwenda ughaibuni, wengi walimpiga mawe kwamba alichemka.
Papo kwa hapo (leo) nikapata jibu pasi shaka late kachero mbobezi hakukimbia kampeni ila ilikuwa ni issues za kiafya.
Maisha yetu binaadamu ni kificho kwetu na afya zetu ni hazina ambayo kila mtu anajijua alivyo ni mwenyezi Mungu tu ndiye anapanga na kupangua.