Rasmi Lomalisa amalizana na Yanga anaenda kucheza soka Uarabuni kuanzia msimu ujao

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Beki huyo wa kushoto wa Yanga amemalizana na klabu yake hiyo baada ya kumalizika kwa msimu wa 2023\2024
Ambapo uongozi wa Yanga walitaka kumpa mkataba mpya wa mwaka mmoja lakini Lomalisa aliomba kuondoka klabu hapo nakwenda kutafuta changamoto mpya.

Lomalisa ambaye amecheza kwa mafanikio ndani ya misimu miwili ndani ya timu hiyo ya Yanga ikiwemo kuisaidia Yanga kubeba mataji ya ligi kuu ya NBCPL na FA

Na sasa Uongozi wa Yanga wameanza kutafuta mbadala wake ambaye anayezungumziwa ni Beki ya kushoto ya kazi kutoka Asante Kotoko ya Ghana Ibrahimu Imoro.

 
Thank you Jocye Lomalisa, Waziri wa Maji. 🙏

Wakati unasajiliwa, nakumbuka baadhi ya mbumbumbu walikukejeli sana kutokana tu na hili jina lako. Ila baada ya kuwawashia moto uwanjani, kejeli zote zilikwisha!
 
Hii week pia, Rasmi Joseph Guede anamalizana na Yanga. Wakitua dar yeye na Lomalisa wanafata release letter zao.
 
Mbadala wake anafahamika siku nyingi tu. Thankyuuu Lomalisa Mutambala, siku hizi hueleweki unapiga krosi mbayaaaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…