Sio kwa awamu hii, mbona wengine sisi hatujasumbuliwa na ni mashomire? Tatizo alikuwa mpigaji na mjanja fulani hivi, ukienda hapo ofisi za tff karibu nafasi zote muhimu zimekamatwa na sisi wa Kanyigo, Nshamba, Kamachumu, zisizo muhimu ndio wa huko Upareni, Mwandiga, na Wambulu wanazishikilia. Jamaa alitaka kuhamishia ofisi kwenye jengo ghali na katikati ya jiji lakini wadau wakapaza sauti. Mwenye roho ngumu tu anaweza kufanya hivyo sio roho za kimchezo mchezo. Hivi kwa akili ya kawaida Malinzi uchaguzi huu angeshindwa kweli wakati alishawalambisha wajumbe mikwanja ya kitakatishaji kitambo? Awamu hii ipo makini, haitaki ujanja ujanja wa Kimagomeni Magomeni.