Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 819
- 1,093
Mkurugenzi wa kampuni ya toka The Look Ltd Basila Mwanukuzi amekabidhi umiliki wa uandaaji wa mashindano ya Miss Tanzania kwa kampuni ya Lamata Village Entertainment inayomilikiwa mwongoza filamu nchini Leah Mwendamseke 'Lamata'.
Aliyekuwa mmiliki wa Miss Tanzania, Basilla Mwanukuzi (kulia) akibadilishana mkataba na Mkurugenzi wa kampuni ya Lamata Village, Lamata Leah,jijini Dar es Salaam leo,katikati ni mwakilishi wa BASATA,Abel Ndaga. Picha na Michael Matemanga
Makabidhiano hayo yamefanyika leo Aprili 14,2025 Mlimani City Dar es Salaam ambapo yatamruhusu Lamata kuendesha shughuli za shindano hilo la kuwapata warembo nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Lamata Village, Grace Mgaya amesema wanatambua uzito wa jukumu walilokabidhiwa na kuahidi kushirikiana na wadau kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa viwango vya juu.
"Huwezi kulitaja jina la Lamata bila kutaja ubora. Tuna hamu kubwa ya kuona Miss Tanzania inarejea kwa nguvu na heshima yake," amesema Mgaya.
Mtayarishaji wa filamu ya Jua Kali, Leah Lamata, amesema: "Mimi sio mzungumzaji sana lakini nitayathamini, nitayaongoza na kuhakikisha mashindano ya Miss Tanzania yanatoa kilicho bora zaidi.
Ikumbukwe awali mashindano hayo yalikuwa yanasimamia na marehemu Hashim Lundenga tangu mwaka 1994 hadi 2018 ambapo alimuachia kijiti Basila Mwanukuzi.