Rasmi, Nigeria yatangaza kuuza mafuta yake kwa kutumia sarafu yake ya Naira badala ya Dola Marekani

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Nigeria, nchi tajiri kwa mafuta na gesi barani Afrika, imetangaza pia kuwa itaanza kuuza mafuta ghafi kwa sarafu ya ndani badala ya dola ya Marekani, ambayo bado inatumika sana katika biashara za kimataifa za bidhaa.

Tangazo hili la hivi karibuni linakuja baada ya nchi kadhaa kuanza kuuza mafuta na gesi kwa sarafu za ndani kufuatia kuzuka kwa mgogoro wa Urusi na Ukraine mnamo Februari 2022.

Mohammed Manga, mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma katika Wizara ya Fedha, alitangaza kupitia taarifa siku ya Jumapili kwamba Baraza la Mawaziri la Shirikisho (FEC) limeagiza kuwa mauzo ya mafuta ghafi yafanywe kwa naira.

Manga alibainisha kuwa hatua hii ya kimkakati inatarajiwa kuwa na athari ya kudumu kwenye uchumi wa Nigeria kwa kuongeza ukuaji, utulivu, na kujitosheleza kiuchumi.

Alisisitiza kuwa Nigeria bado inapitia changamoto za masoko ya kimataifa na kwamba hatua hii ya kimkakati inaweka nchi hiyo kwenye nafasi ya kufanikiwa siku zijazo.

Nigeria ina hifadhi ya mafuta ghafi inayokadiriwa kuwa mapipa bilioni 37, ikiwakilisha asilimia 3.1 ya hifadhi ya mafuta duniani.

Nigeria ni mojawapo ya nchi 15 bora duniani kwa uzalishaji wa mafuta ghafi, ikiwa na hifadhi ya nane kwa ukubwa na ni nchi ya sita kwa usafirishaji wa mafuta duniani.

Source: AA

1728461520175.png
 
Hahaha ya Sisi hizo Naira tutazitoa wapi?
Waongo tu hao wanajazana upepo, hata Nigerians hawayaki Hizo Naira, wana zibadili kwa dollor na kutunza dollar.
Wanajidanganya kwa muda mfupi na kujipa matumaini tu.
Utazinunua Naira kwa dola benki kuu ya Nigeria ndipo ununue mafuta yao

Watapata faida mara mbili kukuzia Naira na kukuuzia mafuta

Hiyo itapandisha thamani ya Naira ya Nigeria

Wako sahihi sana kwa hiyo hatua
 
Nigeria, nchi tajiri kwa mafuta na gesi barani Afrika, imetangaza pia kuwa itaanza kuuza mafuta ghafi kwa sarafu ya ndani badala ya dola ya Marekani, ambayo bado inatumika sana katika biashara za kimataifa za bidhaa.

Tangazo hili la hivi karibuni linakuja baada ya nchi kadhaa kuanza kuuza mafuta na gesi kwa sarafu za ndani kufuatia kuzuka kwa mgogoro wa Urusi na Ukraine mnamo Februari 2022.

Mohammed Manga, mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma katika Wizara ya Fedha, alitangaza kupitia taarifa siku ya Jumapili kwamba Baraza la Mawaziri la Shirikisho (FEC) limeagiza kuwa mauzo ya mafuta ghafi yafanywe kwa naira.

Manga alibainisha kuwa hatua hii ya kimkakati inatarajiwa kuwa na athari ya kudumu kwenye uchumi wa Nigeria kwa kuongeza ukuaji, utulivu, na kujitosheleza kiuchumi.

Alisisitiza kuwa Nigeria bado inapitia changamoto za masoko ya kimataifa na kwamba hatua hii ya kimkakati inaweka nchi hiyo kwenye nafasi ya kufanikiwa siku zijazo.

Nigeria ina hifadhi ya mafuta ghafi inayokadiriwa kuwa mapipa bilioni 37, ikiwakilisha asilimia 3.1 ya hifadhi ya mafuta duniani.

Nigeria ni mojawapo ya nchi 15 bora duniani kwa uzalishaji wa mafuta ghafi, ikiwa na hifadhi ya nane kwa ukubwa na ni nchi ya sita kwa usafirishaji wa mafuta duniani.

Source: AA

View attachment 3119697
Kutoka kwenye mfumo wa dollar kwa sasa ni ngumu unless kuwe na umoja mkubwa kama brics etc, peke yako hivi ni kudanganyana, hao viongozi tu utakuta wana dola wameficha nje
 
Mafuta yanawabeba na yana soko kubwa
Ukiyataka nenda na dola zako benki kuu ya Nigeria nunua Naira kisha hizo Naira nunua mafuta yao

Wako sahihi
 
ubaya mifumo mingi ya hela duniani kote marekanj ndio anacontrol , na anafanya chochote msitoke kwenye mfumo ikiwemo kuongeza tarrifs etc, watajaribu watarudi tu kwwnye dollar utakuja kuniambia, huwezi kuachiwa utoke kwenye mfumo kirahisi hivyo
 
Ngoja tuone lakini binafsi naiona ni hatua nzuri
 
Nchi zote zinapenda ili kuboost hela zao tatizo mifumo iliyowekwa na mabeberu ni migumu kutoka, mfano nilituma hela kwenda japan kunuanua gari ,nashangaa ikapita wiki hela haijafika
Kwenda bank nikaambiwa hela zimekwama new york kwa corresponding bank, wameomba more information about you, nikatuma after 2 weeks ndio zikafika japan, just imagine hela unatuma kutoka tanzania kwenda japan lakini marekani ndio anaamua zifike au zisifike
 
Sasa kama bado unatakiwa kwenda na dola ya kimarekani kwenye benki kuu ya Nigeria eti ndio ubadilishiwe wakupatie hayo madafu yao ndio ukanunulie mafuta, mbona bado ni dola ileile inatumika.

Hizo ni siasa tu za kitoto hamna anayeweza kuacha kutumia dola kwenye biashara ya kimataifa.

Majuzi tu tumeagiza mashine moja toka China na tumetumia dola ya kimarekani kwani Proforma Invoice ilitumwa kwamba tulipe kwa dola ya kimarekani na hatukuona Yuan ya China.

Haya mambo ya kusema watu wanaachana na dola ya kimarekani kwenye biashara ya kimataifa ni uongo mtupu. Halafu itakumbukwa kwamba mataifa yanadaiwa madeni kwa dola na yanatakiwa yalipe sasa yataachaje kutumia dola.😯😯
 
Utazinunua Naira kwa dola benki kuu ya Nigeria ndipo ununue mafuta yao

Watapata faida mara mbili kukuzia Naira na kukuuzia mafuta

Hiyo itapandisha thamani ya Naira ya Nigeria

Wako sahihi sana kwa hiyo hatua
Hahaha hata wa Nigeria ujinga huo hawataukubali.
Hao hata vi movie vyao hutumia dollar kwenye pesa, sasa ndiyo ije kwenye biashara?

BRICS inawadanganya watarudi tu.

Basi waruhusu matafa makubwa yatengeneze hixo Naira yazimwage humo uswahilini kwa kununua hayo mafuta, uone kasheshe lake.

Watakulana nyama.
 
Nchi zote zinapenda ili kuboost hela zao tatizo mifumo iliyowekwa na mabeberu ni migumu kutoka, mfano nilituma hela kwenda japan kunuanua gari ,nashangaa ikapita wiki hela haijafika
Kwenda bank nikaambiwa hela zimekwama new york kwa corresponding bank, wameomba more information about you, nikatuma after 2 weeks ndio zikafika japan, just imagine hela unatuma kutoka tanzania kwenda japan lakini marekani ndio anaamua zifike au zisifike
Yawezekana kuna uongo mahali
Wengine hushilikilia pesa wawekeze kwanza ndipo watume Either hiyo benki yako au hiyo correspondence bank

Lakini Transfer hutakiwa iwe faster
 
N kama kujitekenya na kucheka yan unaenda na dola unapewa naira una nunua mafuta
Sio kujitekenya hiyo hatua itapandisha thamani ya Naira

Nenda hapo Afrika kusini tu dolla huwa hawataki wanataka ununue bidhaa zao kwa Rand

Unanunua Rand kwa dola ndio ununue bidhaa zao kwa Rand
 
Utazinunua Naira kwa dola benki kuu ya Nigeria ndipo ununue mafuta yao

Watapata faida mara mbili kukuzia Naira na kukuuzia mafuta

Hiyo itapandisha thamani ya Naira ya Nigeria

Wako sahihi sana kwa hiyo hatua
Hizo hatua wauziane wenyewe humo ndani na Naira zao, international trade zina masharti mengine.

Watamuuzia urusi na China hayo mafuta?

Wape muda utasikia.

Masikini huwa tukishiba tuna lala tunasahau njaa huwa ina rudi tena kwa kasi sana.
 
Back
Top Bottom