Rasmi, Nigeria yatangaza kuuza mafuta yake kwa kutumia sarafu yake ya Naira badala ya Dola Marekani

Rasmi, Nigeria yatangaza kuuza mafuta yake kwa kutumia sarafu yake ya Naira badala ya Dola Marekani

Sasa kama Russia kaweza kwanini sisi tusiweze ni swala la muda TU madhari lonauwezekano wa kufanyika litafanyika TU hata kama litachukua muda kiasi gani. Pili ni china nae kafanya hvy

Mkuu jana hapa China ametoa misaada ya mitungi ya kupikia 800 kwa Tanzania.

Yaani kama mitungi ya gesi tu tunasaidiwa what makes you think we can get rid of the dollar?
 
Watanzania bana sijui tukoje! Nigeria ndio wameamua kutumia mfumo huo kwa malengp ya kuimarisha sarafu yao,watanzania tunapinga tunasema haiwezekani! Hawa watu wamekaa chini wametathimini wakaona inawezekana ndio maana wakatoa tangazo. Sisi tunaongea maneno matupu kuwa haiwezekani.

Uzuri wameongelea ununuzi wa mafuta ghafi tu sio kila bidhaa itafanyika kwa naira. Na hawajasema kuwa wanaitupilia mbali dola bali wanafanya biashara ya ya mafuta kwa naira.

Ikitokea wamejaribu na wasifanikiwe, bado wataonekana ni majasiri sababu wamedhubutu tofauti na sisi ambao hata kujitambua tu ni shida. Tuwape moyo wanapojaribu kujitoa kwenye makucha ya hao wanyonyaji sio kuwakatiksha tamaa.

Mkuu kwenye ukweli tuseme.

Nigeria inaitegemea Marekani vibaya sana. Mwaka 2022 walipokea karibu 1,2 Billion USD from US kama grants and aid.

Hivi unadhani nchi inayokusaidia hivyo inaweza kukubali usitumie currency yake?

Watu hawasemi kwamba Nigeria imekosea kwa uamuzi wao but REALISTICALLY haiwezekani.

Na huo ndio ukweriiiiiiiii
 
Kikubwa Dola Moja ni naira ngapi

au ,naira Moja sawa na TSH ngapi haikijaathirika kitu
 
Ka move on su kabanwa?

Akilegezewa vikwazo anarufi mbio.

Mfungwa kukwambia tuliisha zoea na kufurahia maisha gerezani haimaanishi hapendi uhuru.
Inamaanisha ka adopt hali anayolazimishwa kuiishi.
Tatizo unafikiria Russia ni Zimbabwe. 2 years hawatumii dollar + 17,000 economic sanctions lakini uchumi wao bado unakua. Iran hatumii $ na ana vikwazo, niambie kuna nchi Africa ya kushindana nayo kiuchumi?.

Wenzetu wana watu wenye IQ kubwa za kuongoza nchi, sio kama kwetu huku kila kitu uchawa $ imefika 2,800.
 
Marekani kama super power wa dunia ameweka mifumo yote ya kukopesha ,kutoa huduma etc kwa dollar
TAnzania na third world countries tuna import almost everything, jusi nimeshangaa kumbe hadi nondo za kujenga sky scrappers tuna import achana na bidhaa nyingine za ujenzi, kwa hiyo yule ghorofa obviously atapiga mahesbu yake kwa usd ili apate faida baada ya kuinvest
Serikali inakopa kwa dollar na ili ilipe itabidi iwe na reserve kubwa bot ya dollar kuweza kulipa madeni yake na kuwezesha kuimport bidhaa kwa wananchi wake maana dollar ndio major currency inayotumika kwenye soko la kimataifa, leo hata ukitaka kitu china mchina atakupa quotation ya dollar
Kwahiyo demand ni kubwa mno mno
Umejibu vema, lakini hapo kwa mchina umepuyanga. Sahivi unaweza kulipia Tshs to Yuan, hata gari kwasasa sio lazima ulipie kwa $, ukitaka kwa japanese Yen unalipia fresh kabisa.

Dunia inaenda kubadilika chief, Dunia haitabaki kama zamani.
 
hoja ya nigeria ni ukusanyaj wa fedha za kigeni ili kupata wepesi kufanya transactionna sio kukimbia dola...moja yafaida ni kukuuwa kwa pesa yaoambpo kawaida uchumi unakuwa,,pia uagizaj wa bidhaa kutoka nje utakuwa ni mwepesi.
 
Tatizo unafikiria Russia ni Zimbabwe. 2 years hawatumii dollar + 17,000 economic sanctions lakini uchumi wao bado unakua. Iran hatumii $ na ana vikwazo, niambie kuna nchi Africa ya kushindana nayo kiuchumi?.

Wenzetu wana watu wenye IQ kubwa za kuongoza nchi, sio kama kwetu huku kila kitu uchawa $ imefika 2,800.
Wabungo wana mahaba sana na usa huwaambii kitu utasikia ni mamtoni huko juu na humemwewbii kitu kuhusu usa
 
Sio kujitekenya hiyo hatua itapandisha thamani ya Naira

Nenda hapo Afrika kusini tu dolla huwa hawataki wanataka ununue bidhaa zao kwa Rand

Unanunua Rand kwa dola ndio ununue bidhaa zao kwa Rand
Wewe ndio bonge la ignorant, unafahamu wakati wa utawala wa makaburu dola moja ilikuwa sawa na rand ngapi na leo wanapotawala hao waswahili exchange rate ikoje.

Angalia Russia toka aondolewe kwenye SWIFT thamani ya sarafu yake imekuwaje. Ikitokea upungufu wa dola unajua nchi zinavyohangaika kulipia madeni yao au hujui.
 
Tatizo unafikiria Russia ni Zimbabwe. 2 years hawatumii dollar + 17,000 economic sanctions lakini uchumi wao bado unakua. Iran hatumii $ na ana vikwazo, niambie kuna nchi Africa ya kushindana nayo kiuchumi?.

Wenzetu wana watu wenye IQ kubwa za kuongoza nchi, sio kama kwetu huku kila kitu uchawa $ imefika 2,800.
Hata uelewi chochote kuhusu hizo nchi. wale ni wazalshaji wakubwa wa mafuta duniani. Urusi ina reserve kubwa sana ya Dollar, na hata Iran unadhani mafuta wanauza kwa madafu?
Angalia Ruble exchange rate yao, unadhani nani atakaa na makaratasi yale.
Nyie ndio washangiliaji hata kama timu inafungwa.
 
Kama kawaida ya akili ya Africans iliyojaa mavi , sasa wamempa Dangote sole exclusive rights ya kuuza jet fuel full 💯 monopoly, mbwa sana hawa wanajimaliza kwa ujinga tuu☹️
 
Sio kujitekenya hiyo hatua itapandisha thamani ya Naira

Nenda hapo Afrika kusini tu dolla huwa hawataki wanataka ununue bidhaa zao kwa Rand

Unanunua Rand kwa dola ndio ununue bidhaa zao kwa Rand
Kwanini tusinunue Rand kwa Tsh wakati Africa Kusini ni ndugu zetu na tuliwasaidia katika harakati za ukombozi?!
 
Sasa kama bado unatakiwa kwenda na dola ya kimarekani kwenye benki kuu ya Nigeria eti ndio ubadilishiwe wakupatie hayo madafu yao ndio ukanunulie mafuta, mbona bado ni dola ileile inatumika.

Hizo ni siasa tu za kitoto hamna anayeweza kuacha kutumia dola kwenye biashara ya kimataifa.

Majuzi tu tumeagiza mashine moja toka China na tumetumia dola ya kimarekani kwani Proforma Invoice ilitumwa kwamba tulipe kwa dola ya kimarekani na hatukuona Yuan ya China.

Haya mambo ya kusema watu wanaachana na dola ya kimarekani kwenye biashara ya kimataifa ni uongo mtupu. Halafu itakumbukwa kwamba mataifa yanadaiwa madeni kwa dola na yanatakiwa yalipe sasa yataachaje kutumia dola.😯😯
Wewe unabishana na Nanani?Wao ndo wameona hivo marekani anafanya biashara ya Dora nchi nyingi zimeshituka walianza European union na wengine watafuata
 
Wewe unabishana na Nanani?Wao ndo wameona hivo marekani anafanya biashara ya Dora nchi nyingi zimeshituka walianza European union na wengine watafuata

Back
Top Bottom