Rasmi sasa Madereva wa malori wa Tanzania wanaishia mpakani, magari yanapulizwa dawa anachukua dereva wa Rwanda. Hatuaminiki tena

Rasmi sasa Madereva wa malori wa Tanzania wanaishia mpakani, magari yanapulizwa dawa anachukua dereva wa Rwanda. Hatuaminiki tena

Hawa wapuuzi wamechinjana sana.. sisi tumewatunza kama wakimbizi miaka mingi..

Ila wao corona kidogo tu wanatubagua.. na hapo hapo utakuta hawawazuii wachina kuingia rwanda au waitaliano

Kwa hiyo unataka wapelekewe corona.

Sisi tunajifanya vichwa ngumu,acha tutengwe tu.
Na bado kama tutendelea kuchukulia simple hili suala kuliona kama
series au movie tutaengwa zaidi hata kama maambukizi yakiisha.
 
View attachment 1436238

HALI ILIVYO RWANDA: Dereva wa Lori kutoka #Tanzania haruhusiwi kuvuka Mpaka wa Rusumo ili kuepuka kuingiza Corona nchini humo.

Badala yake; akifika kituo cha Kiyanzi, mzigo wote utapuliziwa dawa kisha atakabidhi Lori kwa dereva wa Rwanda ambaye atalipeleka hadi kituo cha mwisho. Serengeti Post on Twitter
Hivi sisi nani alitushauri ??!!. Mbona hatuakisi jina letu la Tanzania !!!

Odhis *
 
Sawa, na atakaetoka nalo Rwanda aishie hapo hapo mpakani, gari lipuliziwe dawa kisha achukue dereva wa Tanzania na alifikishe hadi kituo cha mwisho, hakuna kuaminiana hapa
 
Hapo napata mashaka je mzigo ujipote au gari kuharibika nani atakuwa responsible ku cover hizo garama.
Pili itachukuwa mda gani gari ya huyo davo kurejea boda aliko achwa
Kama uliwanza haya ilitakiwa ufuate kanuni za afya za kimataifa....vinginevyo ndio hivyo
 
Nchi yoyote iliyoshuhudia mauwaji ya watu wengi iwe kwa vita au kimbari ..genocide huwa inajua uchungu wa kupoteza wapendwa wao watafanya kila njia kuepuka shida ya namna hiyo
 
mkorinto,
Waoneni mnavyo waona ila; Wameamua kuwalinda raia wao. Eleweni kuwa weshawafungia mipaka hivyo wewe ka dere patania mzigo hadi mpakani ukiisha ufikisha, rudi home ukalingojee gari lako ukiwa home.

Likiisha rudishwa mpakani, kalichukue. Tamaa ya kumletea tajiri hela nyingi itakuponza ufie huko ka yule mwenzenu. Nasema, mipaka imefungwa kabisaaaa hivyo usitagfute lawama
 
Mi naogopa Jamaa wanaweza kimtibua akazuia ma maize kwenda 254...., sisi wakulima tutauza 3000 debe, huwa akikasirika tunaumia peasants wake !!!!
 
Ni jambo la kheri kuchukua hatua ila kiuhalisia kama Tz ingesitisha hadi usafirishaji wa mizigo kutoka port hao jamaa wangekuwa kwenye hali mbaya mno.

Pengine kuna bidhaa muhimu zingeadimika sokoni mapema tu.

I can't imagine kwa mizigo inayopitia Mombasa Kenya to Kigali Rwanda kama utaratibu ni huuhuu.
 
mkorinto,
Waoneni mnavyo waona ila; Wameamua kuwalinda raia wao. Eleweni kuwa weshawafungia mipaka hivyo wewe ka dere patania mzigo hadi mpakani ukiisha ufikisha, rudi home ukalingojee gari lako ukiwa home.

Likiisha rudishwa mpakani, kalichukue. Tamaa ya kumletea tajiri hela nyingi itakuponza ufie huko ka yule mwenzenu. Nasema, mipaka imefungwa kabisaaaa hivyo usitagfute lawama
kuna maisha nje ya corona yanaendelea,corona ni fulsa pia lwa baadhi ya watu.

hivyo msiwe na mtizamo huo 100% mtaingia shimoni,mambo yakiendelea kuwa mabaya.

leo kwao kesi ni 83,mipaka imefungwa.kesho akisikia kuna case 200 hakawii kusema kuna watz wanatorokea kwake huyu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo Rwanda Rusumo boarder naomba nikujibu hivi;

1. Rwanda hawana figisu za kuchakachua mizigo na kupiga minyoka ya mafuta kama bongo. Very disciplined!

2. Gari likiharibika wanawasiliana na mmiliki atapendekeza gerage gani ipelekwe na atalipia kama ambavyo dereva wenu angelipia.

3. Itachukuwa muda ule ule ambayo ingemchukuwa dereva wa Tanzania. 2 to 3 days. Consignments za Rwanda zinakuwa cleared online kabla mzigo haujafika, hakuna urasimu wa kitoto.

Overall; mna uhuru pia kuacha kuleta mizigo, au kufunga mipaka.
Haya ni maamuzi ya HE. PK, HE M7 and HE UK.

Sent using Jamii Forums mobile app
hapo border mahnd $ mchele bei gan kwa kilo moja?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rwanda ina wafanyabiashara wengi wenye malori yanayoijia mizigo tz mojakwamoja yanayoendeshwa na warwanda wenyewe naona kabisa wanajiumiza wao wenyewe
 
Back
Top Bottom