Rasmi sasa Tabora United imekuwa TRA United SC

Hivi huku ligi za chini si kulikuwa na timu ya TRA au kumbukumbu zangu haziko sawa.
Ni kama nilikuwa naona kwenye makampuni ya kubeti.
 
wajinga kweli yaani kodi zetu wana nunua timu. kwanini wasianzishe timu halafu waipandishe ili kupunguza gharama.

au kama vipi wanunue timu ambayo haiko ligi kuu ili waipandishe tuone kama wako siriazi na hela za walipa kodi
Walikua nayo ila naona wameona wanachelewa

Pia sishangai CG Mwenda alikua muanzilishi was timu ya KMC kipindi Yuko Meya manispaa ya Kinondoni ..jamaa anaipenda Yanga , anapenda mpira
 
Hivi huku ligi za chini si kulikuwa na timu ya TRA au kumbukumbu zangu haziko sawa.
Ni kama nilikuwa naona kwenye makampuni ya kubeti.
Ndio ilikua inacheza First Division imeshindwa kutusua wameona Bora wanunue timu ya ligi kuu
 
wajinga kweli yaani kodi zetu wana nunua timu. kwanini wasianzishe timu halafu waipandishe ili kupunguza gharama.

au kama vipi wanunue timu ambayo haiko ligi kuu ili waipandishe tuone kama wako siriazi na hela za walipa kodi
Kuanzisha timu ipande madaraja hadi ligi kuu ni gharama kubwa sana, inaweza kuchukua hata miaka 20.
 
Nafikiri hii timu haitamaliza hata msimu tangu kununuliwa kwake.

Maana baada ya ukombozi tu kupatikana tunaifutia kabisa usajili.

Eti TRA sports club pumbavu kabisa.
 
Sasa walikuwa wanapinga nini..

Lakini wanangu hizi pesa zilizonunua tabora united si ndio kodi zetu.
Hivi TRA ina mfuko wa kufanya manunuzi ya kitu chochote kile hata chupi au soksi za kamishina wa tra?

Hivi tumefikaje hapa na huu wendawazimu?

Nani amepitisha matumizi au manunuzi ya timu kwa uhalali upi?

Hawa watu unajua wanatudharau sana?
 
Tra waachane na hii biashara ya mpira ni hasara, Kodi tunayolipa isielekezwe huku
Mimi ninachohoji nani atakuwa analipia gharama za huu umalaya wa kiuchumi? Nani atalipa makocha, wachezaji mishahara, na gharama za kambi nani?

Tangu lini mamlaka ya usimamizi na ukasanyaji wa mapato ikajipa umuhimu wa kuwa na timu ya mpira?
 
Kila kitu Dar! Iende hata Arachuga kwa machalii
 
Aisee acha tu hadi mtu unafika point unakosa maneno.
 
Kuna uhusiano gani wa kuwa na timu na kuhamasisha kulipa kodi
Ni sawa na kutumia kampuni ya Bia kama TBL au Serengeti au K-Vant kuhamasisha afya ya figo.

Sasa wana hamasisha kulipa kodi kwa kutumbua kodi nani atakuwa audience ya huu upumbavu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…