Rasmi sasa Tabora United imekuwa TRA United SC

Rasmi sasa Tabora United imekuwa TRA United SC

Yaani TRA kwa makudi kabisa mnaamua kuzichezea kodi zetu! Nyinyi wenyewe mnazichezea na kuzitafuna kila siku! Wanansiasa nao wanazitafuna vile wapendavyo kwa kununua magari yao ya kifahari, nk! Na sasa mnazipeleka na kwa wachezaji nao waazitafune!

Yaani sisi wafanyabiashara tunahangaika kutafuta juani, halafu nyinyi wenzetu mliopo kivulini mnatumbua tu kodi zetu! Hivi kulikuwa kuna umuhimu kweli wa kuingia kwenye hii biashara!!
Hapo Kinyerezi hivi majuzi watumishi wa TRA walikuwa wanapita kwa wakina mama wanauza mahindi barabarani na wachoma mishikaki mida ya jioni, eti wanaomba leseni ambayo gharama yake ni 50,000/= na kama huna leseni walikuwa wanakujua wanakupeleka kituoni staki shari...

Hebu imagine wewe unafanya kijibiashara cha kuchoma mahindi ambacho mtaji wake haufiki hata 20,000/= halafu unaambiwa eti ukate leseni ya 50,000/= kama huna hiyo hela unanyang'anywa biashara na kisha unaswekwa ndani...

Haya hujakaa sawa unakuja huku mitandaoni unakutana na habari kama hii eti TRA sasa hivi wanaendesha timu...aisee inauma sana.

Hakika hii nchi inahitaji kufanyiwa total overhauling, ngoja tu tupate uhuru kamili.
 
Ni jambo jema tulizaliwa zamani kidogo hili sio jambo geni, zamani tulikuwa na Reli ya Morogoro, RTCKigoma, CDA Dodoma, Tanesco, Mecco, Maji Dodoma, nk
 
Why sasa wanunue nyingine?
Kuitoa timu majalalani kule league one mpaka ligi kuu sio kazi nyepesi.
Yaani watoke league one kisha championship ambako kuna ushindani wa kufa mtu, then wavuke waje ligi kuu!
 
Mimi ninachohoji nani atakuwa analipia gharama za huu umalaya wa kiuchumi? Nani atalipa makocha, wachezaji mishahara, na gharama za kambi nani?

Tangu lini mamlaka ya usimamizi na ukasanyaji wa mapato ikajipa umuhimu wa kuwa na timu ya mpira?
Kabla ya kununuliwa nani alikuwa analipa? Au timu zingine zinapata wapi hela, mfano
KMC
JKT
MASHUJAA
SINGIDA BS
MBEYA CITY nk
 
Ingebaki huko huko Tabora, na jina pia lingebaki Tabora United inayomilikiwa / kufadhiliwa na TRA.
 
Back
Top Bottom