Rasmi: Tanzania yaipiku Kenya kwa gharama za miradi baada ya miaka 35

Rasmi: Tanzania yaipiku Kenya kwa gharama za miradi baada ya miaka 35

Kwa muda wa zaidi ya miaka 35, Kenya imekuwa ikiongoza kwa Afrika Mashariki katika maendeleo na uandikishaji wa miradi mipya. Ni katika miaka ya 2016-2017 Ethiopia ikaingia katika kusuguana na Kenya katika gharama za miradi iliyoandikishwa na serikali zao. Lakini kwa mara ya kwanza kutoka katika ripoti ya kampuni ya kimataifa deloitte imeonyesha kwa mwaka 2019, Tanzania ama walikuwa wakiita the sleeping giant imepindua meza kwa kuweza kusajili miradi mikubwa 51 yenye gharama ya 61.3 billion usd sawa na Tzs Trilioni 150.hii ni sawa na asilimia 41% ya miradi inayoendelea katika nchi za Afrika Mashariki. Nchi ya Kenya imekuwa ya pili kwa kusajili miradi 51 yenye jumla ya thamani ya dola billioni 30 billion USD ama Tzs Trilioni sabini sawa na asilimia 24% ya miradi inayoendelea Afrika Mashariki. Tanzania imekuwa na miradi inayoendelea kama Standard Gauge, bwawa la umeme, mchuchuma ama lng plant, ilihali Kenya imeendelea katika miradi ya Standard Gauge, treni, barabara. Ripoti hii imezihusisha nchi zilizoko Afrika Mashariki ambazo ni Burundi, Djibouti, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Rwanda, Shelisheli, Somalia, Tanzania na Uganda.
 
Back
Top Bottom