Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imesema inaendelea kuchunguza ukwepaji kodi kupitia udanganyifu wa taarifa za magari, ikiwemo aina, modeli, mwaka wa kutengenezwa na thamani ya gari.
TRA imesema katika operesheni iliyofanyika Septemba 26, 2026, eneo la Palm Beach Casino, Dar es Salaam, ilibaini gari aina ya Mercedes-Benz G-Wagon lililokuwa bila namba za usajili.
Kwa mujibu wa TRA, nyaraka za forodha zilionesha gari hilo kuwa Mercedes-Benz G-Class G350, mwaka 2020, huku uchunguzi wa kitaalamu ukibaini kuwa ni Mercedes-AMG G63, mwaka 2018, yenye thamani kubwa zaidi.
TRA imesema gari hilo lililosajiliwa kwa jina la Omary Faraji Nyembo limekamatwa na uchunguzi unaendelea, huku hatua za kiutawala, madai ya kodi au kisheria zikichukuliwa kulingana na matokeo ya uchunguzi.