Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Akiongea na BBC Swahili hivi karibuni, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu hatimaye amezizungumzia tetesi na tuhuma zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii kwamba CHADEMA wana hulka ya kujiteka wenyewe ili wapate huruma ya wananchi.
Kwenye mahojiano hayo, Lissu amegusia sakata la Chacha Wangwe ambaye kwa muda mrefu sasa, limekuwa ni gumzo kutokana na tetesi zilizosambaa kuwa kada huyo wa CHADEMA aliuliwa na chama chake.
Kuhusiana na sakata hilo Lisssu amedokeza kuwa tuhuma hizo si za kweli na kwamba kama ingekuwa ni kweli basi wangechunguzwa.
Tundu Lissu aliongeza kwa kusema:
Soma pia: Tundu Lissu: Vyombo vya Usalama haviwezi kujichunguza vyenyewe sakata la Mauaji na Utekaji nchini

"Nilianza kuyasikia miaka mingi sana. Marehemu Chacha Wangwe aliuliwa na CHADEMA. Hii sio habari mpya. Kama ni kweli nani katika nchi hii na sheria ipi ya nchi inayosema kwamba CHADEMA wana ruhusa ya kuuana? Ni sheria ipi inayosema kwamba CHADEMA wakiuana, jeshi la Polisi haliwezi kufanya uchunguzi?"
Tundu Lissu aliongeza kwa kusema:
"Haya maneno ni aidha ya wauaji wenyewe au wapambe wao. Hizi si maneno ambazo zinapaswa kutiliwa maanani na mtu yoyote mwenye akili"
Soma pia: Tundu Lissu: Vyombo vya Usalama haviwezi kujichunguza vyenyewe sakata la Mauaji na Utekaji nchini