Alexandry Nemesi
JF-Expert Member
- Jun 7, 2014
- 1,507
- 589
Ratiba Kamili Ya Uchaguzi Wa CHADEMA Taifa.
Katibu Mkuu anawatangazia wanachama wote kuwa kutakuwa na uchaguzi wa viongozi wa Chama na Mabaraza kwa ngazi ya Taifa utakaofanyika Januari, 2025.
Fomu za kuomba kugombea nafasi za uongozi ngazi ya Taifa zinapatikana ofisi za Makao Makuu ya Chama, Makao Makuu ya Mabaraza, Ofisi za Kanda, Ofisi za Chama za Mikoa na Wilaya kuanzia tarehe 17/12/2024. Mwisho wa kurejesha fomu ni tarehe 05 Januari, 2025 saa 10:00 jioni katika Ofisi za Makao Makuu ya Chama Mikocheni, Dar es Salaam au katika Ofisi za Kanda anayotoka Mgombea husika. Aidha Wanachama wanaogombea katika Mabaraza ya Vijana, Wanawake na Wazee watatakiwa kurejesha Fomu hizo katika Ofisi za Makao Makuu ya Mabaraza ya Chama zilizoko Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, Dar es Salaam au katika ofisi za Kanda anayotoka mgombea husika.