Hivi, mwanamke akiwa na mimba changa anapenda sana kufanya mapenzi , kiufupi hamu yake ya kufanya mapenzi inaongezeka zaidi kipindi hiki. Kwaiyo wala husiwe na wasiwasi, fanya tu uwezavo wala hatosema basi, ila atafurahia tu. Na kama haukufanya nae, basi utamchanganya akili na ugomvi utaanza. Hiyo hata vitabuni imeandikwa, nenda kamulize dokta atakuelewesha vizuri. Sababu mwili wa mwanamke una change hata ubongo wake pia unachange.
Ila mimba ikifika miezi 4-5, ile hali ya kupenda kufanya mapenzi mara kwa mara inabadirika kwake. Sababu tumbo linakuwa kubwa na anajiona mzito na mvivu wa kufanya lolote lile, na hata kufanya mapenzi ataona uvivu, tabu na uzito. Vile vile tumbo kubwa linazuia kufanya mapenzi, kwaiyo ataona bora ahache kufanya uwo mchezo, kwanza anaumia mkandamizo. Kwaiyo ukitaka kufanya nae mapenzi uwe mjuzi kweli kweli na uelewe tatizo lake, tena umshawishi kitaalam haswa, kama si hivo utanyimwa kila siku kaka yetu. Hapo ujue kubembeleza, ukifos, umekwisha. Labda ukatafute kismall house, na hiyo ndio itasababishe ndoa yako ife kabisa.
La kufanya: Wajuzi wanasema tumia mda mwingi sana kwa mkeo, wanawake wajawazito ujiskia wapweke sana na uwa na mawazo yasio simulizika. Naskia wanaota ndoto za ajabu ajabu, kuhusu mtoto alie tumboni. Ila hawasimuli mtu. Ukiwa nae shika shika tumbo lake tu, maana pale ndio penye tatizo. Kama kumwambia ebu nikupake mafuta tumboni mke wangu, heheh. Au kumwambia tumbo lake linang`aa na umelipenda. Au unamsaidia kazi za home. Unamfulia mara moja moja, na kumpikia. Ukimshauri apumzike. Mwanamke akiwa mjamzito tumbo kubwa hawezi kuinama, kwaiyo kazi za kuinama home ukimsaidia, itakuwa msaada mkubwa kwake. Hata kama ukaona anaweza kufanya kila kitu na anakukatalia husimsaidie, we msaidie tu na mwambie unamuonelea uruma na hali alio nayo.
Ukimuacha na tumbo, na kazi zote peke yake, na unajifanya hauna time wala muda wa kukaa nae, basi hata yeye atajiskia haumjari kwa vile ana mimba, atakuona ni mtu mbaya, ham na wewe atokuwa nayo, na ugomvi utakuwa hauishi, na mwisho kuchukiana. Kwaiyo hata akizaa ile chuki kwako itakuwepo, wala hato kuamini na wala hato kupenda tena kama zamani. Hiyo ndio ratiba ya maisha ya ndoa.