Haha, nacheka kwasababu ni Uhuru Kenyatta mwenywe ndio anapanda majukwaani na kusema atafanya kazi kama JPM.
Uhuru miaka 6, JPM 2½ halafu unataka kiwalimgamisha. 43% ya watoto walio kuwa wana shindwa kwenda shule za msingi kwa kikosa ada, leo wanaenda shule. Upande wa sekondari hiyo ni 10%.
Umeme unakusudiwa kufika zaidi ya ya 3500MW ndani ya miaka miwili. Bandari inachimbuliwa hivi sasa, leo hii reli za meter gauge ambazo hazijatumika kwa takriban 30yrs zimefufuka na zingine zinakarabatiwa. Wafanyakazi hewa 19,000, wakurugenzi wa mashirika mishahara imepumguzwa, ufufuaji wa mashirika makuu ya usafiri na mawasliamo. Zowezi zima la rushwa, kubwa na ndogo, rada za ndege za abiria nchi nzima, mikoa 7 inajengewa wodi maalum ya watoto wachanga. Vituo 12 vya ukusanyaji damu nchini, vitanda mahospitalini, bado sijagusia hospitali za rufaa zinazo jengwa mpya. Upande wa mageuzi ya kimfumo, mabenki, mashirika ya umma, tawala za mikoa, kuhamia Dodoma, ukusanjaji wa kodi, hati za viwanja, mabadiliko ya sheria za madini, kukaa chini na kujadilia na wachimbaji wa madini wakubwa. Yote hii ni ndani ya miaka 2½, na wala sijaweka vitu ambayo JPM amerithi kutoka serikali ya Kikwete.