Simiyu Yetu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2013
- 18,949
- 4,639
Baada ya jana jioni bunge la katiba kuingia katika hali ya sintofahamu iliyochangiwa pia na wabunge wa chadema,cuf na nccr- mageuzi leo asubuhi bunge litaendelea na shughuri zake kama inavyoonesha hapa chini.
1. Kuanzia saa tatu asubuhi mwenyekiti wa bunge maalumu mh samweli sitta ataweza kuwaapisha wabunge waliosalia kuapa ambao idadi yao yapata kama thelathini hivi.
2. Baada ya wabunge hao kumaliza kuapa jaji warioba ataweza kuwasilisha rasimu ya pili ya katiba ambapo imepangwa kuanza saa tatu na nusu au na dakika arobaini na tano mpaka saa saba kamili mchana.
3. Baada ya warioba kumaliza kuwasilisha rasimu mwenyekiti atalieleza bunge nini kitafuata baada ya zoezi hilo kukamilika.
Hivyo ndivyo utaratibu utakavyokuwa kwa leo karibu sana tuendelee kufuatilia katiba yetu inavyotungwa.
Samahani wakuu hiyo tarehe ni 18-3-2014 mkono uliteleza kidogo.