Ratiba ya Chakula na Vinywaji ' Msibani ' pande za Oysterbay ipoje?

Ratiba ya Chakula na Vinywaji ' Msibani ' pande za Oysterbay ipoje?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Mnaogawa Vyakula na Vinywaji tunaomba katika ile Sufuria ya Nyama muwe mnawaachia Sisi Waombolezaji wenyewe ndiyo tuwe tunajipakulia kwani wengine tukipakuwa huwa tunapakuwa vya Kula Siku Mbili Tatu huku Majumbani mwetu Uswahilini.

Na hakikisheni kuwa pale mkiwa mnaanza zamu ya kugawa Vinjwaji muwe mnarudia rudia kila baada ya Nusu Saa lakini kama itatokea kutakuwa na Pombe kama ulivyo Utamaduni wa Marehemu hasa kwa Kabila lake tunaomba mtuachie tu Waombolezaji tuwe tunajichagulia tu wenyewe idadi ya Bia au Wine za Kuchukua.

Kama kuna Mtu ana Ratiba kamili hasa ya Chakula na Vinywaji naomba aniwekee hapa tafadhali.

Nawasilisha.
 
Kufa kufaana kwa kweli. Nipo makumbusho ngoja nisogee eneo la tukio.
 
mkuu,, hiyo slope itakutokea puani, ukija huku mikoani usipende kula misibani,utakula punda
 
Kuna kijiji fulani ulitokea msiba, ikapikwa Kande,wanakijiji wakagombea balaa, baadae yakatolewa masinia ya ubwabwa nyama, watu walitamani kutapika

Ha ha ha ha ha ha ha.....Mkuu umezitesa mno Mbavu zangu kwa Kicheko.
 
Sababu za kuondoa msiba masaki ni zipi?naomba kufahamu
 
Back
Top Bottom