itategemea na ratiba yako zaid mkuu na ulaji wako, ila mimi nakushauri hivi.
J3. chai/maziwa + chapati 1/2 kulingana na ukubwa, mtori na chapati moja, supu, (au vyovyote upendavyo) mana inategemea je unapika au unaenda ktk mgahawa
Lunch: kula wali + mboga upendayo. Dinner: Ndizinyama + unaweza ukawa na kikombe cha chai/juice
J4: chai/maziwa + kitafunwa, supu, au mtori, au tambi + chai
Lunch: Ugali + mboga upendayo + mboga ya kijani. Dinner: Viazi nyama + mboga ya kijani - (juice, chai)
J5: Chai fuata mtiririko hapo juu + kitafunwa upendacho
Lunch: tambi zipike vizuri + maharage yaliyoungwa vizuri tamu sana hii kitu, au nyama ya kukaanga kidogo + chai/maziwa
Dinner: Pata wali/pilau (kama pilau utaweza itakaa vizuri sana) +mboga nzuri + mboga ya kijani
J6: chai as per the above.
Lunch: futali uipendayo iliyoungwa vizuri na tamu.
Dinner: Ugali + mboga nzuri + mboga ya kijani
J7: Chai amua tu plz vitafunwa ni wewe mwenyewe au supu au mtori nk.
Lunch: ndizinyama + maharage yaliyoungwa vizuri, tamu sana.
Dinner: pata pilau ya motooo kula lala.
J8: chai amua
Lunch: kama unaweza tafuta kitu simple ule, ndizi mzuzu + nyama kidogo, tambi + nyama choma, ukishindwa pata Ugali + mboga uipendayo + mboga ya kijani.
Dinner: Viazi nyama + maharage + mboga ya kijani.
J9: mtori /supu + chapati
Lunch: Makande please.
Dinner: ugali/wali/pilau.
NB: Kumpangia mtu ratiba ya msosi ni kazi nzito sana, mfano hapo ingekua mme wangu ungeinjoy maana ningepanga
hata ubloo, pia kuna baadhi ya vyakula sijaweka cozi nina wasiwasi we ni dume unaweza kuona ni kazi tu. pia
wengi tumekalili sana mchana ugali, usiku wali.
ila jitahidi usirudie chakula mara kwa mara, cha msingi jitahudi kwa wiki umekula walau vyakula vyovyote kwa
hivi vya kawaida, ukiachana na vile vya kihoteli hoteli zaidi.
wasalimie.