Ratiba ya PlayOff ya ligi kuu Tanzania bara, unatabiri yapi kutokea ?

Ratiba ya PlayOff ya ligi kuu Tanzania bara, unatabiri yapi kutokea ?

Timu 2 za daraja la chini zimepanda moja kwa moja - Kengold ya Mbeya na Pamba ya Mwanza.

Timu 2 za Ligi kuu zimeshuka moja kwa moja - Mtibwa ya Morogoro na Geita Gold ya Geita

Hizi playoffs zina lengo la kuongeza ushindani ligi kuu, timu 2 za ligi kuu na moja ya ligi ya chini zinashindana kuwania nafasi mbili za kurudi / kupanda ligi kuu, timu dhaifu inashuka / kurudi ligi ya chini.
Umetoa ufafanuzi mzuri. Na wadau wa michezo wanatakiwa waelewe siyo mara zote timu za Ligi daraja la kwanza zimekuwa ni dhaifu.

Na mfano mzuri ni msimu uliopita pale Mbeya City iliposhushwa Ligi kuu na Mashujaa Fc katika mtoano wa aina hii.
 
Mwaka jana ilikuaje?
ligi kuu vs championship, (kulikua na game 4, i.e kila timu ilicheza home and away ila walizikutanisha timu za ligi kuu na zile za d1)

kulikua na mbeya city vs mashujaa
na nyingine sijui ilikua nani na nani......
 
Sasa hapa kushuka mbona ngumu Ivi.

Ilitakiwa playoffs wacheze wale wa daraja la Kwanza wao Kwa wao,

hawa WA kutoka logo kuu wangeshuka moja Kwa moja
 
Mashujaa kuiondoa mbeya city na pia Ihefu kuiondoa mbao fc
Mbao kwanza ilipanda bila kuwa na sifa (iliokota dodo)
Mbao haikuwa na uongozi(ilikuwa na watawala)

Mbeya city kulikuwa na msuguano mkali wao kwa wao (viongozi)

Mashujaa yalikuwa maagizo ya cdf kuhakikisha timu hii inapanda(marefa wanajua nini walikuwa wanaambiwa)

Vaibu la mashabiki wa mashujaa

Umoja wa wazee wa ujiji pamoja na waganga wote wa kigoma na nchi jirani walikuwa wapo kigoma kuhakikisha mashujaa inapanda

●Mashujaa walikuwa na mkakati kabambe wa kuhakikisha hakuna timu itawai kupata ushindi pale lake Tanganyika(bahati nzuri walivurugana wao kwa wao that why kuna muda mashujaa walichezea vipigo haswa)

○mashujaa imepoteza mvuto kiasi Fulani kwa wana mkoa baada ya mkuu wa kikosi ambae kiasili ni muha kwenda masomoni na kikosi kuwa chini ya mzenji ambae now anajaza wazenji wenzake
 
haya mambo ya playoff ya kupanda na kushuka ni ya kipuuzi sana, tuache kuiga kila kitu.
 
Back
Top Bottom