Ratiba yako ya kwenda 'Site' ni ipi?

Ni wiki nyingine ya mchaka mchaka. Tukimbizane na mishe zetu hadi wikiendi tupate chapaa ha kwenda kupiga hatua site. Tusikubali unyonge vijana.

Sisi tupo tu. Tunawasubiri.

Wale wanaohitaji mbao, mzigo tunao wa kutosha. Sogeeni tu maeneo au tupigieni simu tuyajenge.
 
Hapo mwisho sijaelewa,unaposema Futi 20,halafu ukaweka 2*2 = 400 unamaanisha nini hapo
 
Mkuuu mbao za blandaring munauzaje?
 
Wajibu wetu ni kuwakumbusha tu. Wikiendi imeshafika. Mnaenda site au kidimbwi? [emoji3]
 
Hivi muda mzuri wa kwenda site ni upi? Asubuhi au jioni?
 
Siku hizi mnajikausha sana ila wikiendi si ndio hii? Swali letu liko pale pale.
 
Wikiendi imewadia. Wakati muafaka wa kukagua maendeleo ya ujenzi.

Kama una safari ya 'Site' tupigie simu tukuandalie mzigo wa Mbao imara kwa bei nafuu. Mabati yapo pia.

Au huna hata kiwanja?
 
Wikiendi imefika. Kazi yetu ni kukumbusha na kuhimiza.
 
Wikiendi imefika. Kazi yetu ni kukumbusha na kuhimiza.
Jamaa yangu alikaa kama mwaka na zaidi hajaenda site. Siku hiyo yuko kwenye ki grosare na washkaji wakawa wanamsisitiza awanunulie pombe yeye anadai hana hela.

Jamaa wakamwambia acha kutuzuga wewe, huna hela na huku tunaona karibia unamalizia mjengo pale kwenye kiwanja chako? Jamaa ndio kupanik kesho yake kaenda kakuta kweli jamaa wanapaua mjengo! Twendeni site jamani.
 
Haaaaaaaa madalali wakawa washafanya yao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…