Ratiba yako ya kwenda 'Site' ni ipi?

Hii ngekewa ilinidondokea kwenye Mabati, Nikajisemea kweli Mtembea Bure si sawa na mkaa bure...
 
Pole na hongera sana mdau. Kwenye kupaua ulikutana na changamoto gani?
 
Mimi kabla sijajenga nilinunua Kirikuu ambayo imenisaidia sana kama kupeleka mafundi site, kununua mwenyewe material kama cement nk. Nasimamia ujenzi mwanzo mwisho na wakimaliza jioni nawabeba nawarudisha, hakuna aliyeniibia, zaidi sana mimi nina uelewa wa ufundi hadi ratio za cement nilikuwa nawaelekeza.

Sikuchukua mafundi expensive ila hawa hawa wadogo nilikuwa nawaelekeza navyotaka mimi na sio ushauri wao. Mjengo umeisha na ninaishi himo na familia yangu, kazi nyingi za finishing kama water system, sanitation kama jikoni kuweka marble, kufunga WC (water closet) kupiga gypsm na skimming pamoja na Painting nimefanya mwenyewe!

Nilikuwa nafanya hivi, nikimwita fundi site na nikiona ana gharama kubwa labda kutokana na kazi inahitaji vifaa basi mimi nanunua vifaa hivyo nafanya mwenyewe kazi ikiisha napata faida ya vifaa. MFANO fundi bomba akija anataja gharama yake anaweza kusema kila kupiga thread joint moja ni 500, basi nikanunua Die za bomba pamoja na Vice pamoja na pipe wrench kazi ikiisha vinabaki kuwa vyangu.

Fundi wa mageti nkaona gharama zake ni kubwa anasema kutengeneza geti ni 450,000 basi mimi nanua mashine ya welding ya 280,000 na material za 150,000 nafanya mwenyewe kwa vile naweza kuthubutu, hivyo nimebaki na mashine ya welding na geti nikalishona mwenyewe, hadi sasa nina mashine nyingi za kazi nafanya mwenyewe kurekebisha nyumba pale linapotokea tatizo kwa vile vitendea kazi ninavyo.
 
Mimi kabla sijajenga nilinunua Kirikuu ambayo imenisaidia sana kama kupeleka mafundi site, kununua mwenyewe material kama cement nk. Nasimamia ujenzi mwanzo mwisho na wakimaliza jioni nawabeba nawarudisha...
Duh! Wewe kama mimi tu..ila tu tofauti ni kwamba mimi ni fundi kamili,sikuhitaji kumuita fundi yeyote,mi nikipata hela ya tiles nachukua dukani nakuja kugonga n.k
 
hivyo nimebaki na mashine ya welding na geti nikalishona mwenyewe, hadi sasa nina mashine nyingi za kazi nafanya mwenyewe kurekebisha nyumba pale linapotokea tatizo kwa vile vitendea kazi ninavyo.
Vizuri sana mkuu, sababu kubwa namba 1 inayosababisha tuwatumie mafundi ni ukosaji wa vitendea kazi Vifaa.

Zamani nilikua nikiona meza inacheza cheza namwita fundi anakuja na nyundo na misumari mfukoni anagonga mara mbili tatu Anaondoka na 5000 na 2000 la piki piki hapo nishatumia.

nikaaanzaga kama utani nikanunua nyundo, taratbu nikaja misumeno, mdogo mdogo nikaja na Tape Measure, maraa paap sasa hivi namiliki store yenye vifaaa visivyopungua 5m Vifaa tupu.

Welding machine zipo,Nyundo masururu,mavifaa yote ya Ujenzi ninayo huwa fundi anapokuja kufanya kazi kwangu sharti langu ni 1.

Aingie kwangu akiwa Empty Hand Sitaki kumuona na kibegi wala kipochi, aje na akili yake tu, Tunaingia store namuuliza anataka kifaa gani nampa anatumia anafanyia kazi akimaliza mazaga yangu ananiachia.

Hapa nipo nadunduliza nichukue mashine la kufyatulia matofali na paving..

Kuna faida nyingi sana kuwa na vifaa vyako ambapo faida ya kwanza kubwa inayonifanya kila senti niipatayo nisiache kununua kifaa chochote ni Hela ninazokodishia haya mavitu, Mafundi wakishajua una mashine ya kitu flani nzuriiii wao wenyewe wanakuja kuzikodisha wakafanyie kazi. Visent vya vocha havikosekani.
 
Hongera sana mkuu
 
Mimi kabla sijajenga nilinunua Kirikuu ambayo imenisaidia sana kama kupeleka mafundi site, kununua mwenyewe material kama cement nk. Nasimamia ujenzi mwanzo mwisho na wakimaliza jioni nawabeba nawarudisha, hakuna aliyeniibia...
Wewe kila ufundi unaufaham???au mm ndo cjaelewa

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Duuuuu!! Mwenzetu naona kila ufundi unaufahamu hongera sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…