Ratiba yako ya kwenda 'Site' ni ipi?

Mkuu unajifanya kazi zote unadumaza uchumi, tugawane riziki.

By the way Kuna molding za pavers za kichina zenye maumbo mbalimbali.
Naona kama ni nzuri
 
Mimi kabla sijajenga nilinunua Kirikuu ambayo imenisaidia sana kama kupeleka mafundi site, kununua mwenyewe material kama cement nk. Nasimamia ujenzi mwanzo mwisho na wakimaliza jioni nawabeba nawarudisha,...

Safi sana mkuu
 
Kama ilivyo ada, kila ikifika mwisho wa wiki kama leo tunakumbushana kuhusu site.

Unaenda lini? Unahitaji mzigo wa mbao tukuuzie na kukusafirishia hadi site kwako?

Wasiliana nasi
 
Mimi Kila siku asubuhi na mapema naenda kumwagilia kabla ya kwenda ofisini, na jioni napoludi home napitia ndipo naludi home. Na siku ofisini kukiwa hamna kazi hiyo siku ntashinda na mafundi nawasupport na story za hapa na pale jioni nageuka nao pamoja.
 
Mimi kukiwa na mafundi wanaendelea na kazi huwa nashinda huko, huwa siondoki kabisa. Ila kipindi ambacho mafundi hawapo huwa naenda kila wikiendi, naenjoy tu kushinda huko hata kama hakuna kinachoendelea
 

Safi sana, huu ni utaratibu mzuri. Ukiwa na mahusiano mazuri na mafundi hawatataka kukuangusha!
 
Mimi kukiwa na mafundi wanaendelea na kazi huwa nashinda huko, huwa siondoki kabisa. Ila kipindi ambacho mafundi hawapo huwa naenda kila wikiendi, naenjoy tu kushinda huko hata kama hakuna kinachoendelea

Unashinda nao kwa sababu huwaamini au unataka kujua yanayoendelea?
 
Unashinda nao kwa sababu huwaamini au unataka kujua yanayoendelea?
Hapana mkuu, sio kwamba siwaamini bali ni sehemu yangu ya kusimamia ujenzi wa nyumba yangu, kwa upande mwingine kwangu ni hobby. Faida inayopatikana ni pamoja na kuwarekebisha wanapokosea maana huwa nipo makini sana, kazi zangu huwa sipendi ziwe na makosa ya kijinga kijinga, mfano, fundi wangu haikutumia pipe level wakati wa kumimina msingi, matokeo yake wote mnajua kuwa msingi haukuwa level moja. Ili kurekebisha hili nilimbana sana atumie pipe level kwenye kupandisha top kozi na nilibaini kutofautiana kwa upande mmoja na mwingine kwa zaidi ya centimeter kumi! Hili ni kosa ambalo usipoliona mapema lazima litakuja kuonekana baada ya kupaua na fundi wa ujenzi ushamlipa na ashasepa!
 
Wakuu naombeni mnipe mawazo
Nna site nmeshajenga kiti
Vyumba vitatu vyakulala moja ni self,sebule na min store na choo na bafu...
Sasa kifusi chakujaza pale juu naona ni karibu trip kadhaa...
Trip moja ni kaka 65000! Nkawaza hapa naweza maliza hata 500000 kwa kifusi tu...
Nkawaza labda nchimbe kwanza shimo la choo afu ule mchanga niumwage mule ndani...
Sasa kuchinba shimo mzee akaniambia itabid nilifukie kabisa ili lisititie!!!!! Ah nkabak nmeduwaa tena sababu pale hata maji sijavuta bado... sasa nfanyaje njenge shimo au niagize tu kifusi au au au
 
Mwanangu hizi bei za mwaka gani mbona zimepanda sana!!![emoji848]
 
Bei zimepoa kiongoz kidog ckuiz
2×4 bei 5700
2×2 bei 2800
1×8 bei 13000
1×10 bei 17000
Ok sawa labda inategemea unachukulia wapi.
Ila bei zilizopo sokoni hiz hapa chini
2×2=2200
2×4=5000
1×6=5000
1×8=10000
1×10÷14000
 
Nilikutana na dilema hii, niliamua kununua kifusi na kilinigharimu kama 1.2M pamoja na kujaza kwenye msingi wenyewe. Sikuchimba shimo kwasababu sikuwa na bajeti ya kujenga na kilikuwa ni kipindi cha mvua hivyo yangelibomoa vibaya sana endapo ningechimba bila kujenga.
 

Dah shida sana
 

Hii hali imenikuta pia na hapa wazo nililonalo ni kuleta vifusi tu vijaze maana hata nikichimba shimo la Choo bado kifusi hakitotosha, kwangu kuna Kuna Mteremko kidogo ambao tofali za upande wa chini zimefika Kozi kumi na mbili.

Vifusi havikwepeki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…