Ratiba za masomo kuongezewa muda wa masaa mawili kutakuwepo na malipo ya ziada kwa walimu?

Ratiba za masomo kuongezewa muda wa masaa mawili kutakuwepo na malipo ya ziada kwa walimu?

Mnasihi

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2013
Posts
7,762
Reaction score
7,100
Waziri wa Elimu katia waraka na ratiba mpya za mihula ya shule jana.

Ndani ya waraka huo kaongeza muda wa masaa mawili kwenye RATIBA za shule yaani zianze SAA 2:00 asubuhi hadi SAA 10:00 jioni badala ya SAA 8:00 mchana.

Katika kuongeza huku hakuzungumzia malipo ya ZIADA (overtime) kwa walimu ambao no watekelezaji na wasimamizi wa RATIBA hiyo.

Nauliza je, amesahau kuwa muda wa kazi kwa mwajiriwa wa umma unaishia SAA 9:30 alasiri? Kama kaongeza muda wa kazi haoni kuwa Kuna haja ya kumlipa ZIADA huyu mwalimu kwani naye muda wake wa kazi hautofautiani na wafanyakazi wa kada nyinginezo?

CWT na hata serikali watoa majibu ya kama KUTAKUWEPO na malipo ya ziada na kinyume chake kutaleta mgogoro wa kikazi kati ya mwajiriwa na mwajiri.
 
wakati watoto wapo nyumbani si walikuwa wanalipwa? hizo pesa ndio wanazifidia sasa
Mimi ni mwalimu. Wakat watoto wapo nyumbani nilikuwa natoa kazi watoto wafanye na nasahihisha madaftar karibua elfu moja kwa wiki. Hilo lilikuwa agizo la katibu tawala wa mkoa niliopo.

Sasa hayo masaa mawili ya ziada yapo kisheria na posho inatakiwa iwepo. Vinginevyo naona kama wanapigia mbuzi gitaa. Sina mpango wa kukaa mpaka muda huo. Mm ikifika saa 7 mchana nachora nipo geto.
 
Walimu bwana; miezi mitatu mmelipwa bila kufanya kazi hata lisaa limoja leo mnahoji kuongezewa masaa mawili?

Kwa kukufanunuliwa masaa ya kufanya kazi kisheria ni 40 - 45 kwa wiki. Kama unaingia kazini saa 1.30 mpaka Mpaka saa 10-30 jioni ukiondoa lisaa limoja la mapumziko ya chakula utakuwa umefanya kazi masaa 8 hivyo kwa wiki masaa 40 ambayo yako kisheria.
 
Hili laweza kuwa jibu kwangu kwa nilichokutana nacho nikiwa mzazi

Uongozi wa shule (binafsi) unatutaka wazazi kuzibeba -bank pay slip za muhula wa pili, tunapowapeleka watoto wetu. Nikamuuliza mbona mhula wa pili haujaisha?

Akasema hata wakati wa hili janga walimu wao walikuwa wanawalipa,. Nikajiuliza hivi mzazi anatoa ada ili Mwl. alipwe au ili mtoto afundishwe nikaweka busara ya kutohoji maana najua uhalisia wa uendeshaji wa hizi shule (Ni karo)

Hili laweza kufidia muda lakini ubora wa elimu wanafunzi watakayopewa kunawalakini

Kulipwa naona wasilipwe maana wakati wa janga walilipwa bila kazi .. Maana ulikuwa wakati wao kujishughulisha na mambo yao
 
Mimi sioni tatizo maana shule nyingi hasa za gvt watoto hutoka SAA nane na nusu wwkati muda wa kazi no SAA tisa na nusu, hivyo walimu tunaiibia serikali SAA limoja, sasa kufikia SAA 10 na nusu ni saa limoja tu limeongezeka

Changamoto iko kwa watoto hasa sisi tunaofundisha vijijini ,mtoto ataweza kukaa darasani kwa almost teni hours bila kula? Maana shule nyingi ni za kutwa

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni mwalimu. Wakat watoto wapo nyumbani nilikuwa natoa kazi watoto wafanye na nasahihisha madaftar karibua elfu moja kwa wiki. Hilo lilikuwa agizo la katibu tawala wa mkoa niliopo.

Sasa hayo masaa mawili ya ziada yapo kisheria na posho inatakiwa iwepo. Vinginevyo naona kama wanapigia mbuzi gitaa. Sina mpango wa kukaa mpaka muda huo. Mm ikifika saa 7 mchana nachora nipo geto.
Ukiondoka utovu wa nidhamu ... Ukiwa T.O.D utaamua kuondoka au la!
 
Hili laweza kuwa jibu kwangu kwa nilichokutana nacho nikiwa mzazi

Uongozi wa shule (binafsi) unatutaka wazazi kuzibeba -bank pay slip za muhula wa pili, tunapowapeleka watoto wetu. Nikamuuliza mbona mhula wa pili haujaisha?...
Mzazi anatoa ada ili mtoto afundishweamalize syllabus kwahiyo kama wataimaliza lazima ulipe kiasi chote kinachopaswa kulipwa.
 
Saa kumi mbona kawaida tunakaa na watoto mpaka saa nne usiku hakuna hizo sijui nyongeza hiyo sawa tu sema kupiga hii pasi ndefu mpaka desemba ndo ishu
 
Ukiondoka utovu wa nidhamu ... Ukiwa T.O.D utaamua kuondoka au la!
Ndugu yangu. Nilianza kazi ya ualimu katika hizi shule za kata za serikali nikitokea shule ya private. Kama unavyojua shule za private ni nginja ngija.

Mnaamka saa 12 asubuhi mnawasimamia watoto katika program mbali mbali hadi saa 4 usiku wanakwenda kulala. Mshahara ulikuwa mzuri mixa na viposho na tubahasha twa hapa na pale.

Nilipo kuja serikali nikaendelea na ule moto. Waalim niliowakuta wakaniambia dogo uta sizi kama sio kufleti. Aisee sikuchukua hata miez 6, nikawa kama wao.

Hayo matamko yanaishia kwenye vyombo vya habari. Njoo huku kijijini uone waalim wanaenda shuleni saa 4 asubuhi, yaan ni shidaaa tena kuna siku hatuendi kabisa shuleni nashinda shamba nalima.

Siwezi kujila. Kama posho ipo napiga mzigo kama haipo saa 7 mchana nachora
 
Saa kumi mbona kawaida tunakaa na watoto mpaka saa nne usiku hakuna hizo sijui nyongeza hiyo sawa tu sema kupiga hii pasi ndefu mpaka desemba ndo ishu
Nadhani upo private. Kama upo serikali upewe tuzo. Maana nyie ndo bado waalim kwenu ni wito. Mm nasema ualimu ni kazi kama kazi zingine. Weka ofa mezani tupige kazi. Hakuna ofa utachonga viazi.
 
Kwa kukusaidia tu usipende kuanika plan zako kama umekusudia kufanya hivyo fanya kimya kimya usijekuingia matatani
Mimi ni mwalimu. Wakat watoto wapo nyumbani nilikuwa natoa kazi watoto wafanye na nasahihisha madaftar karibua elfu moja kwa wiki. Hilo lilikuwa agizo la katibu tawala wa mkoa niliopo.

Sasa hayo masaa mawili ya ziada yapo kisheria na posho inatakiwa iwepo. Vinginevyo naona kama wanapigia mbuzi gitaa. Sina mpango wa kukaa mpaka muda huo. Mm ikifika saa 7 mchana nachora nipo geto.
 
Walivyokuwa wapo majumbani walilipwa mishahara ya bure , je ulilalamika kwann wanalipwa bila kufanya kazi?
 
Je, vipi kuhusu wanafunzi hasa shule za vijijini wataweza kuvumilia njaa Hadi hiyo jioni ? Shule nyingi za gvt huko vijijini wanafunzi hawapewi hela ya kwenda kula shuleni tofauti na mijini.

Mfano mwanafunzi anatembea masaa mawili kufika nyumbani na shule ametoka saa kumi. Huoni ni kumtesa huyo mwanafunzi.

Bora ungewekwa utaratibu kwa mda huu uliobaki wawe wanakula mchana shuleni
 
Walipwe overtime ya nini, mbona wamelipwa miezi mitatu bila kufanya kazi, na mwezi wa tatu walifanya nusu mwezi wakalipwa full[emoji848]
 
Back
Top Bottom