Raw food is the new oil

Raw food is the new oil

Ezekiel will

New Member
Joined
Oct 22, 2018
Posts
3
Reaction score
2
Habari wana jamii forum ..!!

Tagu kuanza kwa janga hili la corona "COVD-19" mambo mengi pia yanaendelea kutokea na kushangaza ulimwengu.

Moja ya mambo hayo ni kuendelea kuporomoka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia ambapo leo hii bei ya mafuta imeweka rekodi ya kuporomoka kwa 40% hadi kufikia $10.9 kwa pipa ambayo kwa pesa za kitanzania ni kama TSh 25000 hivi.

Wakati hilo la mafuta linaendelea bei ya vyakula na bidhaa zingine kama barakoa na toilet paper nazo zinapanda kulingana na kuongezeka kwa uhitaji wake hivi sasa.

Hapa nchini kwetu tumeshuhudia sukari ikipanda bei kutoka Tsh 2800 kwa baadhi ya maeneo hadi kufikia Tsh 4000 mpaka Tsh 6000 kwa maeneo mengine.

Turudi sasa kwenye vyakula vya nafaka "RAW FOOD" kama vile mahindi mchele nk.

Bidhaa hizi ndizo zinaongoza kwa uzalishaji wa vyakuka na pia kutumiwa kama chakula kikuu kwa maeneo mengi hapa duniani.

Hapa nchini kwetu, mahindi na mchele ndio vyakula vikuu na hili halina ubishi hata kidogo. Gunia la mahindi kwa bei ya wastani ni Tsh elfu 80 mpaka Tsh laki moja na ishirini (120k) . Kwa namna hii basi, leo hii bei ya gunia moja la mahindi hapa Tanzania ni mara nne ya bei ya pipa moja la mafuta($10.09) kwenye soko la dunia.

Je hii inaashiria nini huko tuendako ?? Je mmiliki na mkulima wa shamba kwa sasa ndio atakuwa tajir pekee hapo badae ?? Vp kuhusu uwezekano wa kupanda zaidi kwa bei ya vyakula?? Je masikini sisi tusiokuwa na kipato ndio mwisho wetu wa maisha ??

Basi tufanye nini sasa ?? ..nini serikali yetu ifanye ?? Wewe na mimi ni hatua zipi tuzichukue sasa ??

Lakini pia mwenendo huu ndio unamaanisha chakula cha nafaka ndio mafuta ya baadae hapo kesho "IS IT TRUE THAT, RAW FOOD IS A NEW OIL ??

kwa huu uwelewa wangu mdogo nimeamua kuleta swala hili hapa jamvini tulijadili ili tupate mawazo chanya ..tujengane na tuelimishane ili sote tuvuke salama mto huu wenye mamba wakali ulioko mbele yetu.

Ahsante.

IMG_-qxf3ey.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom