Ray C amfutia mashtaka Chid benz

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
WAKATI nyota wa muziki wa Hip Hop , Rashid Makwiro ' Chid Benz ' akikamatwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere akiwa na madawa ya kulevya akiwa njiani kuelekea Mbeya, Rehema Chalamila ' Ray C ' aliyekuwa amemfungulia kesi ya kumpiga katika kituo cha Polisi cha Oysterbay, amefuta shauri hilo na kumsamehe.

Akipiga stori na gazeti hili , Ray C alisema ameamua kumsamehe kwa sababu yeye ni mtu wa Mungu na anaamini yanayomtokea ni ishara ya kumtambulisha kuwa matumizi ya dawa za kulevya hayafai . "Mimi ni mtu wa Mungu , nimemsamehe na wala sitaki kesi naye , lakini kumsamehe mimi peke yangu hakusaidii , Watanzania wote kwa pamoja tumuombee ili jambo hili limalizike na likiisha, ninamuomba aje tushiriki pamoja katika tiba ya Methadone, " alisema .

Ray C maarufu kama kiuno bila mfupa, alitoa kauli hiyo muda mfupi baada ya kuandika waraka katika akaunti yake kwenye mtandao wa Instagram, akimsihi Chid Benz kuachana na matumizi hayo ya madawa ya kulevya . Nyota wa muziki wa Hip Hop , Rashid Makwiro ' Chid Benz' . "Pole kaka yangu Chid Benz, naumia kuona tatizo ulilokuwa nalo bado haujalitafutia jibu, mimi ni dada yako na tumeshafanya kazi pamoja .

Tatizo ulilonalo na mimi nilishakuwa nalo na niliweza kulitatua sababu nilijitambua na kutafuta suluhu, nimejaribu kila njia kukushauri badala yake ukaja na rungu la kimasai na kunitandika nalo nyumbani kwangu , " yalisomeka baadhi ya maandishi yake mtandaoni .

Ray C aliendelea kuandika kuwa kitendo cha kukamatwa kwake na madawa hayo kitakuwa ni jibu zuri kwake kuwa anakoenda si salama na kumtaka abadili njia na kuungana naye kwenye tiba ya Methadone kwani ndiyo kiboko ya madawa ya kulevya. Kamanda Nzowa .

Chid Benz alikamatwa akiwa na kete 14 za madawa ya kulevya pamoja na misokoto miwili ya bangi hadi gazeti hili linakwenda mtamboni , alikuwa bado hajafikishwa mahakamani kukabiliana na tuhuma hizi
 
anatafuta kiki huyu Ray C..ngoja Chid Benz atumikie miaka yake kumi keko atakapotoka ayakute hayo maneno ya aliyoandika aone cha Mtemakuni
# But Chid Benz saizi achomoki kwenye huu msala
 
anatafuta kiki huyu Ray C..ngoja Chid Benz atumikie miaka yake kumi keko atakapotoka ayakute hayo maneno ya aliyoandika aone cha Mtemakuni
# But Chid Benz saizi achomoki kwenye huu msala

Hawa walikuwa wapenzi na itakuw ray c kamwagwa maana kila siku yeye na chid
 
Chidi Benz ni nani nchii hii? Mnasema ni rapa,amerapu nini?nipo New York,naipenda sana Tanzania
 
anatafuta kiki huyu Ray C..ngoja Chid Benz atumikie miaka yake kumi keko atakapotoka ayakute hayo maneno ya aliyoandika aone cha Mtemakuni
# But Chid Benz saizi achomoki kwenye huu msala

Nasikia chid katoka kwa dhamana ya mil moja, kazi kweli
 
Mi nadhan kaenda kutoa ile miliion ngapi vile dhamana
 
chid benz madawa yamemuaribu sana, kauza nyumba kwa mpangaji mwingine nhc ilala flats kaenda kupanga mbezi beach hela iliyobaki sijui ndo kanunua hayo makitu aliyokamatwa nayo maskini,
 
Baada ya Chidi kukamatwa, Ray C anafuta kesi yake kisa kua yeye ni mtu wa Mungu. Siku zote hizo alikua hajijui kuwa ye ni mtu wa Mungu? Au ndo ameokoka juzi juzi baada ya Chidi kukamatwa? Hiki kidemu kina lake jambo.
 
Siku hizi nampenda sana Ray C, yale mashauzi yake na swagga zake za zamani za kidada duu hana.

She's grown up now. Hongera zake kwa moyo huo.
 
Baada ya Chidi kukamatwa, Ray C anafuta kesi yake kisa kua yeye ni mtu wa Mungu. Siku zote hizo alikua hajijui kuwa ye ni mtu wa Mungu? Au ndo ameokoka juzi juzi baada ya Chidi kukamatwa? Hiki kidemu kina lake jambo.

Mkuu...ndio maana penseli ikawekwa ufutio!
 
chid benz madawa yamemuaribu sana, kauza nyumba kwa mpangaji mwingine nhc ilala flats kaenda kupanga mbezi beach hela iliyobaki sijui ndo kanunua hayo makitu aliyokamatwa nayo maskini,

Ile NHC ilala si ya familia? Si anaishi na ndugu zake pale include mama yake? Iweje hauze yeye kama yeye?
 
Hongera Ray C. Wanaomponda wana yao. Wewe umesamehe wangapi? Keep it up dada.

Humu wamejaa wapuuzi kibao. Kwao kila kitu wanakipokea kwa mtizamo hasi. Ni vigumu kuwajua wanataka nini na wanapenda kuwajadili watu badala ya issues... si unajua tena ndo kawaida ya wajinga!!! Badala ya kukijadili alichokifanya Ray C wao wako busy kumjadili Ray C, sasa unategemea kuna watu timamu hapo? Bora hata wame ni wanawake tujue kimoja kwani umbea kwao sunna, tatizo unakuta midume mizima inapiga soga za kujadili maisha ya watu binafsi... yaan ni sheedah!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…