Ray C anahitaji msaada

sifongo

JF-Expert Member
Joined
Jun 5, 2011
Posts
4,896
Reaction score
5,305
Habari Wanajamvi, nilikuwa napitia habari kwenye mitandao nikakutana na habari ya kuombewa msaada kwa dada yetu Ray C, Ndugu John Kitime ameandikka na kuweka namba ya tigo pesa kwa wenye nia ya kumsaidia yule dada apate dawa za matibabu ya kuachana na dawa za kulevya namba yenyewe ni 0655999 700.

SWALI LANGU:
HIVI HIZI PESA WANAZOPATA NA KUTURINGIA HUKU MTAANI KIASI KWAMBA HATA MAISHA YAO YANABADILIKA GAFLA NA KUISHI UTADHANI NI MABILIONEA ZINAISHIAGA WAPI?
HABARI HII IPO KATIKA BLOGU YA MICHUZI.
 
Wantafutie kituo cha matibabu kwanza ndiyo hao wenye vituo waombe pesa. Hizo dawa wanazosema anapewa ni zipi dawa ya utumiaji wa madawa ya kulevya ni kuacha kutumia na kuangaliwa (Rehab) kuhakikisha hurudi kwenye kutumia hayo madawa. Huwezi kutumia dawa ikatatua hilo tatizo bali dawa zitakuuwa tu. Dawa wanazosema wengi zi za vichaa psychiatric kama Abilify ambazo ni za watu wenye kurukwa akili na kwasababu kama kufiwa, kutaka kujiua n.k.
 
Ili kuepukana na hii tabia kwanza anatakiwa akamatwe na aeleze alikuwa ananunulia wapi hayo madawa ili tuanzie na chanzo lakini sio kila siku kusaidia mateja tu huku hawa wauzaji wakiendelea kujinufaisha na hizo fedha wanazopata kwa biashara hiyo.
 
Jamani eeh! Mtaftien mafta ya ubuyu.
 
Reactions: kui
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…