Ray c: chid Benz atozea "JELA"

Ray c: chid Benz atozea "JELA"

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
NYOTA wa Bongo Fleva , Rehema Chalamila ‘ Ray C ’
ambaye hivi karibuni aliripotiwa kupokea kipigo cha
maana kutoka kwa msanii mwenzake , Rashid Makwilo
almaarufu Chid Benz , ameibuka na kudai kuwa
atahakikisha rapa huyo anaozea jela kwa kitendo hicho
alichomfanyia.ii
Akizungumza na gazeti hili , Ray C alisema amejikuta
akipatwa na dhamira hiyo kutokana na msanii huyo ,
licha ya yeye mwenyewe na mama yake kumpigia simu
za kutaka amsamehe , lakini anakana mbele za watu
anapoulizwa, tena hadi redioni .
“Chid na mama yake wamenipigia simu kutaka
nimsamehe lakini ninashindwa kwa sababu akiulizwa
na watu anakataa hajanipiga, sasa kama hajanipiga
anaomba msamaha wa nini, nimekwenda kwao na
polisi kama mara tano lakini haonekani , inaonekana
amejificha sehemu, mimi nasema awaonee haohao
wasiojua sheria , ” alisema msanii huyo ambaye hivi
sasa anaendesha vita dhidi ya matumizi ya madawa ya
kulevya .j
Alipoulizwa kuhusu kauli hiyo , Chid Benz mwenye tuzo
tano za Kili , licha ya kukiri kumpigia Ray C simu
pamoja na mama yake , alikataa kupiga kwa ajili ya
kuomba msamaha kwa sababu hakumpiga msichana
huyo mkongwe katika Bongo Fleva .
“Mimi nimpige Ray C ? Halafu achubuke mguuni? Chid
Benz angempiga angepasuka sura na angevimba kila
sehemu. Yeye anajua nini kilitokea lakini anasema
maneno yasiyokuwepo ilimradi apate huruma ya watu .
Nilishamkataza kuwa karibu na mzazi mwenzangu kwa
kuwa najua kampuni yake haina future .
“Mbona hasemi kama nilishawahi kwenda pale na
kumweleza sitaki na akaniomba msamaha ?
“Mimi sikumpiga , mchubuko alioupata ni mchecheto
wake tu baada ya kujikwaa na kuanguka wakati
akinikimbia , mimi nichukue cheni ? Hayo ni mambo ya
kizamani kwamba mtu ukimpatia sababu unasema
amechukua pesa sijui na nini, siwezi kuchukua cheni ya
Ray C , kwa maisha gani aliyonayo ?
“Anasema nilimpigia simu kumuomba radhi , ni kweli
lakini siyo kumwomba radhi , nilimpigia na kumwambia
tuachane na haya mambo, sisi wote tunaonekana
mateja tu mbele za watu ambao tumeshindwana huko
sasa tunataka publicity .
“Wanaosema mimi ni mkorofi hawanijui , kama ni hivyo
mbona ile kesi ya kumpiga msichana kule Ilala
nimeshinda ?” alihoji Chid Benz.
 
Heaven on Earth Dada rehema anaendeleaje aiseeh ? Toka apate kipigo sijasikia maendeleo yake inabid niende weekend hii nikamuone
 
Last edited by a moderator:
Kweli ugomvi wa mateja mgumu sana kuuelewa. Ngoja niwaangalie zangu wasanii wa kueleweka kama kina Davido....
 
hahaaaa binamu unajua nimecheka sana wakati nasoma thread ya Rehema na Chii.. nitarudi

Ahahah Mimi nakumbuka tu kwichu kwichu ,dah uwa nafurah sana nikikumbuka vitimbi vya rehema

Uje bhana binamu , utupe mautamu
 
Ray c vs tid.. ray c vs chid benz...

Ya majeja tuwaachie mateja wenyewe
 
Sehemu pekee inayomfaa Chid ni jela tu kwa sasa.Akitoka atakua sawasawa.
 
Back
Top Bottom