Ray Kigosi: Thus Why I'm So Wonders

Ray Kigosi: Thus Why I'm So Wonders

He didnt go to school as much as u, its not fair to hiss him. His acquisitive should be encouraged, English is equidistant to education. Sasa akae kimya au aache kabisa kuigiza, sio jambo la kucheka.

Kutumia kiingereza katika sinema za kibongo si tatizo sana hasa kama part anayoicheza mhusika itahitaji hivyo, tatizo ni pale actor wa Kibongo anapoongea broken English, hapo ndipo anapoonekana na mapungufu. Kwanini asiifanyie mazoezi hiyo line ya Kiingereza aliyokusudia kuitumia? Kwanini asiconsult wataalam wa lugha hiyo wakamsaidia kuiconstruct kwa namna iliyo fasaha kabla ya kuitumia kwenye movie? Au bado kama hakuweza kuvifanya vyote hivyo, kwanini asistick tu na Kiswahili?
Tunachukulia makosa kama Hayo kuwa ni mepesi tu kwa vile hiyo si lugha yetu, tunasahau kuwa audience inayofikiwa na hizo movie ni pana sana tofauti na zamani kutokana na mabadiliko ya kiteknolojia na kuwa kuna watu wa kutoka nchi zenye kutumia kiingereza na wanatarajia kauli inayotoka kwenye movie iwe na maana au iwe na mantiki ya aina fulani. Kutokana na hilo ni kuwa, wakati sisi tunachukulia kuwa ni makosa ya lugha kwa vile si yake na tunamjua, wao watasema, yule actor/muandaaji/muongozaji au mtayarishaji wa Script hana akili kwa sababu kinachozungumzwa hakieleweki, hakichekeshi wala kuwa na logic yoyote.
Ukisikia Kiswahili cha Hollywood au South Africa, utapata idea kuwa wanazungumza kitu gani hata kama hakina lafudhi original ya kibongo na si blah blah za zisizo na maana.
 
Huwa nawashangaa sana watu wanaohangaika kutazama maigizo ya kitanzania 'bongo movies'...

Huo muda wa kukaa na kutazama hayo maruerue ni bora niutumie kwenda kugonga mdudu...

Nilishashindwa kabisa, hata kwa kupretend Napenda, siwezi kuziangalia, bora Nisogee bar Nipige safari au Niangalie wanyama au hata history Channel.
 
Back
Top Bottom