Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sweet Science of Boxing.Miezi 6 baada ya Ray 'Boom Boom' Mancini kushinda mkanda wa WBA wa lightweight alitakiwa kuutetea mkanda kwa kukutana na Kim Duk Koo.
Kim, mSouth Korea, hakua akijulikana sana na dunia ila alikua na rekodi ya 17-1-1 huku akiwa ameshinda mapambano 8 kwa KO. Alikua ameshinda mkanda wa Orient and Pacific Boxing Federation na alishautetea mara tatu.
Rekodi hiyo ikamfikisha kua challenger namba 1.
Kim akatakiwa kupunguza uzito ili aendane na uzito wa kukutana na Mancini. Ingawa alikua underdog ila alikua na confidence kumzidi Mancini, ukiniuliza mimi nitakwambia alikua ni Chris Eubank Sr wa South Korea. Kim alikuja Marekani peke yake bila familia yake, mchumba wake alikua na mimba, asingeweza kuja.
Akiwa anahojiwa Kim akasema "Ni ama afe au nife" siku ya pambano ilipofika Kim kabla hajajiandaa na kutoka hotelini akaandika kwenye taa ya pembeni ya kitanda "Kuishi au Kufa"
Pambano zima lilinukia kifo kuanzia mahojiano mpaka raundi ya kwanza ilipoanza, ambapo Kim came out strong na akapokelewa na Mancini ambaye alikuja even stronger.
Pambano lilikua la moto, ilikua hamna kurudi nyuma, ilikua ni:
Kumface mpinzani.
Rusha ngumi.
Jitahidi ukwepe.
Rusha tena ngumi.
There was little technic, but power. Power was everything in this fight.
Kufikia raundi ya 3 Ray "Boom Boom" Mancini akarusha left hook ambayo ilimpata Kim, ila akajiumizq mkono na mkono ukaanza kuvimba.
Raundi ya sita, Gil Clancy, mchambuzi wa CBS akasema "Kuna jambo litatokea. Ama kuna mtu atapasuka kichwa au atamzimisha mwenzake"
Pambano lilikua la kibabe na hamna aliyeonekana kumuogopa mwenzake na hakuna aliyetarajia hili. Raundi ya kumi Kim akakatwa point kwa kumshikilia Mancini na kumtwanga kitasa.
Raundi ya 12 Mancini akaachia uppercut ambayo ilimpata Kim kifuani. Kim akaenda chini ila akatua kwa goti. Jini lilitaka damu, there was no stopping, akainuka na mnyukano ukaendelea. Haikua knockdown kwa sheria za kipindi kile.
Ray Mancini akajikusanya na nguvu kidogo alizobaki nazo na kuzitumia katika raundi ya 13 kurusha ngumi kwa kadri alivyoweza. Alirusha ngumi 44 mfululizo na zote zilimpata Kim. Kim akamkumbatia Mancini na hiyo ni njia pekee alimzuia Mancini.
Refa akawaachanisha. Kim hakuwa amewahi kupigana zaidi ya raundi 12, fatique ilishamkamata, hajiwezi, ila jini lilitaka damu, there was no stopping. So pambano likaendelea. Na raundi ya 13 yote Mancini aliitumia kumuadhibu Kim.
Raundi ya 14 ikaingia na Mancini akamfuata Kim huku amempelekea surprise ya left hook. Ikampata.
Mancini akatupa jab ya kushoto na kulia, zikamkosa Kim, ila kinu kilichofuatia kikampata Kim sawia usoni.
Akayumba kidogo, kisha akaenda chini kama kiroba, akiwa chini akajitahidi kushikilia kamba ili ainuke, akaipata kamba, ila sasa hivi zile ngumi za uso zimemvimbisha uso na haoni vizuri tena. Akiwa nusu kusimama vilevile akayumba tena na tena na tena.
Refa akanotice na kuamuru pambano liishe na ushindi ukawa wa Mancini.
Dakika kadhaa baada ya pambano kuisha Kim akaingia kwenye coma. Akatolewa ulingoni akiwa kwenye machela, akafikishwa hospitali wakagundua damu imevuja kwenye ubongo na kumfanyia operesheni kuondoa damu iliyoganda.
Haikusaidia, Kim alifariki siku nne mbele. Kipindi hichi mama yake alikuja kumuuguza, so mama akashuhudia Kim akifariki ugenini.
Jini likataka damu tena
Miezi 3 mbele mama Kim akanywa sumu, akajiua.
Jini likataka damu tena.
Refa, Richard Green, akajiua kwa kujipiga risasi ya kichwa.
Mancini akaingia kwenye sonona. Anasema "Ukiwa bondia hua unakua na heshima kwa mpinzani wako, namheshimu (Kim) na ana heshima yangu yote. Nilitaka kushinda, lakini sikutaka aumie"
Mwaka 2011 Mancini akaenda kuonana na aliyekua mchumba wa Kim, na mwanae, Jiwan Kim, ambaye hakupata bahati ya kumuona baba yake. Jiwan Kim, daktari wa menk, akamuambia "Siyo kosa lako, usiishi na hiyo hatia"
Baada ya hilo pambano na matukio yaliyotokea, sheria zikatungwa na kuubadilisha mchezo wa ngumi na kua tunavyouona leo.
Kwanza ikaamriwa ikitokea chochote kimegusa sakafu ya ulingo na siyo miguu ya bondia basi hiyo ni knockdown na itahesabiwa.
Ikaamriwa pia bondia akipigwa kwa KO leseni yake itafungiwa automatically kwa siku 45.
Badiliko kuu lilikua ni kupunguza raundi kutoka 15 mpaka 12. Utafiti ulionyesha mabondia wengi walipata majeraha au kuumia kuanzia raundi ya 13 na kuendelea.
Hili pambano lilibadilisha ubondia na likabadilisha maisha ya watu. Tukutane baadaye.
Mabondia wa bongo miyeyusho sana.Mchezo hatari ila unafurahisha kutazama. Siku Francis Cheka anapigwa na Dula Mbabe nahisi ingekua Ulaya Cheka ilibidi akapimwe yaani alianguka kabla Dula hajamaliza kurudisha mkono na kuweka guard
Mwaka huu hii corona imezuia mengi sana.Mwaka huu mwishoni au mwanzoni mwa mwaka 2021 kutakuwa na mapambano makali sana.
Mf:1) Ryan Garcia vs Haney,
2)) AJ vs Kublat Pulev
3)Dillian Whyte vs Povetkin
4)Usyka vs Chisora
5)Fury vs Wilder 3
6)A.J vs (Mshindi kati ya Usyka vs Chisora
7)Fury vs (Mshindi kati ya Whye vs Povetkin)
8)Mshindi namba 6 vs mshindi wa namba 7 kwa ajili ya undisputed title.
Pambano litakuwa zuri sana na litaingiza pesa nyingi sana kutokana na ukubwa wa majina yao japo hapo kuna watu wanauwezo mkubwa sana mfano huyo Usyka ila hana mashabiki wengi.Mwaka huu hii corona imezuia mengi sana.
Mimi natamani AJ na Fury wakutane no matter what
Chisora anaenda kupasuka. Personally namuona ni level za wakina Rahman ni overrated.Pambano litakuwa zuri sana na litaingiza pesa nyingi sana kutokana na ukubwa wa majina yao japo hapo kuna watu wanauwezo mkubwa sana mfano huyo Usyka ila hana mashabiki wengi.
Vyama vikubwa vya ngumi vinafanya juu chini kuwakutanisha hawa watu wawili, mfano WBC wanataka kumpandisha Fury kutoka WBC super champion kuwa franchise champion na Dillian kupandishwa kutoka Interim champion kuwa super champion ili kukwepa ile mandatory fight baina yao.
Sasa shida inakuja Fury akikutana na AJ hakutakuwa tena na undisputed title coz franchise belt bondia hawezi kuvuliwa kwa kupoteza pambano.
Yaah, Wilder kwa Fury hatoboi.Chisora anaenda kupasuka. Personally namuona ni level za wakina Rahman ni overrated.
Ila naona Wilder anatolewa kabisa kwenye equation kama vile hajawahi kuwepo. Ana kazi kubwa kiukweli
Unazungumziaje WBC kumpa Fury Franchise Title na Dillian kupandishwa title kuwa WBC super champion?Chisora anaenda kupasuka. Personally namuona ni level za wakina Rahman ni overrated.
Ila naona Wilder anatolewa kabisa kwenye equation kama vile hajawahi kuwepo. Ana kazi kubwa kiukweli
Ingawa bado haijawa official kwa Fury kua franchise champion as anatakiwa amface mandatory challenger ila ikitokea hivyo mimi naona itakua ni namna ya promoter Bob Aram kutengeneza pesa zaidi. As akifanikiwa itakua ni kumruka Dillian na kwenda kwa AJ moja kwa moja.Unazungumziaje WBC kumpa Fury Franchise Title na Dillian kupandishwa title kuwa WBC super champion?
Sasa kwa mantiki hiyo inamaanisha kwamba kama Fury atampiga tena Wilder na kupandishwa kuwa franchise champion na Dillian kuwa Super champion ,inamaanisha kwamba mechi ya Fury na AJ haitapelekea tumpate Undisputed Champion.Ingawa bado haijawa official kwa Fury kua franchise champion as anatakiwa amface mandatory challenger ila ikitokea hivyo mimi naona itakua ni namna ya promoter Bob Aram kutengeneza pesa zaidi. As akifanikiwa itakua ni kumruka Dillian na kwenda kwa AJ moja kwa moja.
Dillian ameitaka hii fight mpaka akaifuata mahakamani. Na ingawa haipo confirmed kwamba atakua WBC super champion ila naona hatokubali mpaka akutane na Fury ulingoni.
Hahaha kukimbiana pia ni tekniki unajua. Mfano Mayweather kwenye pambano na Pacqiao alisemwa kua amekimbia kimbia lakini Mayweather ni miongoni mwa boxers ambao wana high skills kwenye defenceHili ndio pambano langu la Muda wote...
Hapa Ni highlights
Na hapa Ni full fight
Kama unataka kuona usugu wa watu hapa duniani ingia utazame Hilo pambao. Ingia humo uone Nini maana ya ngumi. Sio mapambano ya watu kukimbiana jukwaana.
Mayweather kwangu sio Best Boxer ....Hahaha kukimbiana pia ni tekniki unajua. Mfano Mayweather kwenye pambano na Pacqiao alisemwa kua amekimbia kimbia lakini Mayweather ni miongoni mwa boxers ambao wana high skills kwenye defence