Ray Mancini VS Kim Duk Koo: Pambano lililobadilisha ubondia

Ray Mancini VS Kim Duk Koo: Pambano lililobadilisha ubondia

Sasa kwa mantiki hiyo inamaanisha kwamba kama Fury atampiga tena Wilder na kupandishwa kuwa franchise champion na Dillian kuwa Super champion ,inamaanisha kwamba mechi ya Fury na AJ haitapelekea tumpate Undisputed Champion.

Maana Franchise belt ,ni belt ya heshima tu ,bondia hawezi kupoteza hata akipigwa K.O na mpinzani wake na hata tuseme Dillian na Fury wapigane na Dillian ashinde bado Fury atabaki kuwa Franchise Champion.

Unaonaje hapa?
Katika boxing hizi taasisi za kuusimamia mchezo ni kama vile hazina meno. Kwa maoni yangu na nilichosoma alichotamka Bob Aram ni kwamba promoter anaweza amua bondia wake akutane na nani, haijalishi kama anayetakiwa kukutana naye ni mandatory ama la.

Mfano, Dillian ni mandatory, lakini Bob Aram kasema hawezi kuacha bondia wake apigane na wapinzani wasio na maana hivyo hii franchise title anataka aitumie kumskip Dillian.

So kwa maoni yangu naona hatutakua na undisputed champion, kama ulivyonotice, as kuna mtu ameskip fight hapa. Miaka mbele watu watakua wanabishana ikiwa fight ya AJ na Fury ilitoa the real undisputed champion.

Ni aibu ila mapromota aibu hawana.
 
Kuna kipindi nilisikia tetesi za ajabu sana , kulikuwa kuna uvumi wa kutaka kuwapambanisha mandatory challengers wenyewe kwa wenyewe halafu wawaache Fury na AJ wapambane [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]kiukweli ni heri ilibaki kuwa uvumi tu la sivyo kingekuwa ni kitu cha ajabu mno kuwahi kutokea.

Ila hata hivyo Dillian Whyte kutoboa kwa Povetkin napo ni mziki mnene.

AJ kutoboa kwa Kublat Pulev na kutoboa kwa mshindi kwa Usyka napo ni mziki.

Ila hata hivyo sheria ya mandatory fight ni kwamba bondia akishapigana mandatory fight moja itabidi akae mwaka mzima ili apigane mandatory fight nyingine, sasa sijajua hii sheria inatoka ndani ya chama husika au inajumuisha kwa vyama vyote maana AJ ana mandatory title defences kutoka chama cha IBF, na nyingine kutoka chama cha WBO .
 
By this time AJ kashajijua kua overconfidence ni tatizo lililomcost kwa Ruiz second fight alijirekebisha.

Labda Usyka, Chisora akienda kwa AJ atapigwa.

Anyway, promoters wanajali pesa mno. Huo uvumi usishangae kuna watu wakauleta into reality.
 
Itakuwa hapendi style yake ya upiganaji.

Mayweather mwenyewe anakwambia, "If style makes fight, and I beat all the styles, then my style is the best style".
Hahaha mashabiki tunapenda watu waende toe to toe, ndiyo maana best fight kwetu utakuta ni ile ya Hearns na Marvin na nyingine kama hizo ila hatujui boxer anarisk vingapi kukubali kwenda toe to toe.
 
By this time AJ kashajijua kua overconfidence ni tatizo lililomcost kwa Ruiz second fight alijirekebisha.

Labda Usyka, Chisora akienda kwa AJ atapigwa.

Anyway, promoters wanajali pesa mno. Huo uvumi usishangae kuna watu wakauleta into reality.
Inawezekana kwa sababu hata huu uwingi wa titles ni njia moja wapo ya kujiingizia pesa.
 
Hahaha mashabiki tunapenda watu waende toe to toe, ndiyo maana best fight kwetu utakuta ni ile ya Hearns na Marvin na nyingine kama hizo ila hatujui boxer anarisk vingapi kukubali kwenda toe to toe.
Ujue mashabiki wa boxing, wakiweza kuelewa tofauti kati ya boxer, swammer na slugger hawatapata shida ya kuelewa mchezo wa boxing.
 
Miezi 6 baada ya Ray 'Boom Boom' Mancini kushinda mkanda wa WBA wa lightweight alitakiwa kuutetea mkanda kwa kukutana na Kim Duk Koo.

Kim, mSouth Korea, hakua akijulikana sana na dunia ila alikua na rekodi ya 17-1-1 huku akiwa ameshinda mapambano 8 kwa KO. Alikua ameshinda mkanda wa Orient and Pacific Boxing Federation na alishautetea mara tatu.

Rekodi hiyo ikamfikisha kua challenger namba 1.

Kim akatakiwa kupunguza uzito ili aendane na uzito wa kukutana na Mancini. Ingawa alikua underdog ila alikua na confidence kumzidi Mancini, ukiniuliza mimi nitakwambia alikua ni Chris Eubank Sr wa South Korea. Kim alikuja Marekani peke yake bila familia yake, mchumba wake alikua na mimba, asingeweza kuja.

Akiwa anahojiwa Kim akasema "Ni ama afe au nife" siku ya pambano ilipofika Kim kabla hajajiandaa na kutoka hotelini akaandika kwenye taa ya pembeni ya kitanda "Kuishi au Kufa"

Pambano zima lilinukia kifo kuanzia mahojiano mpaka raundi ya kwanza ilipoanza, ambapo Kim came out strong na akapokelewa na Mancini ambaye alikuja even stronger.

Pambano lilikua la moto, ilikua hamna kurudi nyuma, ilikua ni:

Kumface mpinzani.

Rusha ngumi.

Jitahidi ukwepe.

Rusha tena ngumi.

There was little technic, but power. Power was everything in this fight.

Kufikia raundi ya 3 Ray "Boom Boom" Mancini akarusha left hook ambayo ilimpata Kim, ila akajiumizq mkono na mkono ukaanza kuvimba.

Raundi ya sita, Gil Clancy, mchambuzi wa CBS akasema "Kuna jambo litatokea. Ama kuna mtu atapasuka kichwa au atamzimisha mwenzake"

Pambano lilikua la kibabe na hamna aliyeonekana kumuogopa mwenzake na hakuna aliyetarajia hili. Raundi ya kumi Kim akakatwa point kwa kumshikilia Mancini na kumtwanga kitasa.

Raundi ya 12 Mancini akaachia uppercut ambayo ilimpata Kim kifuani. Kim akaenda chini ila akatua kwa goti. Jini lilitaka damu, there was no stopping, akainuka na mnyukano ukaendelea. Haikua knockdown kwa sheria za kipindi kile.

Ray Mancini akajikusanya na nguvu kidogo alizobaki nazo na kuzitumia katika raundi ya 13 kurusha ngumi kwa kadri alivyoweza. Alirusha ngumi 44 mfululizo na zote zilimpata Kim. Kim akamkumbatia Mancini na hiyo ni njia pekee alimzuia Mancini.

Refa akawaachanisha. Kim hakuwa amewahi kupigana zaidi ya raundi 12, fatique ilishamkamata, hajiwezi, ila jini lilitaka damu, there was no stopping. So pambano likaendelea. Na raundi ya 13 yote Mancini aliitumia kumuadhibu Kim.

Raundi ya 14 ikaingia na Mancini akamfuata Kim huku amempelekea surprise ya left hook. Ikampata.
Mancini akatupa jab ya kushoto na kulia, zikamkosa Kim, ila kinu kilichofuatia kikampata Kim sawia usoni.

Akayumba kidogo, kisha akaenda chini kama kiroba, akiwa chini akajitahidi kushikilia kamba ili ainuke, akaipata kamba, ila sasa hivi zile ngumi za uso zimemvimbisha uso na haoni vizuri tena. Akiwa nusu kusimama vilevile akayumba tena na tena na tena.

Refa akanotice na kuamuru pambano liishe na ushindi ukawa wa Mancini.

Dakika kadhaa baada ya pambano kuisha Kim akaingia kwenye coma. Akatolewa ulingoni akiwa kwenye machela, akafikishwa hospitali wakagundua damu imevuja kwenye ubongo na kumfanyia operesheni kuondoa damu iliyoganda.

Haikusaidia, Kim alifariki siku nne mbele. Kipindi hichi mama yake alikuja kumuuguza, so mama akashuhudia Kim akifariki ugenini.

Jini likataka damu tena

Miezi 3 mbele mama Kim akanywa sumu, akajiua.

Jini likataka damu tena.

Refa, Richard Green, akajiua kwa kujipiga risasi ya kichwa.

Mancini akaingia kwenye sonona. Anasema "Ukiwa bondia hua unakua na heshima kwa mpinzani wako, namheshimu (Kim) na ana heshima yangu yote. Nilitaka kushinda, lakini sikutaka aumie"

Mwaka 2011 Mancini akaenda kuonana na aliyekua mchumba wa Kim, na mwanae, Jiwan Kim, ambaye hakupata bahati ya kumuona baba yake. Jiwan Kim, daktari wa menk, akamuambia "Siyo kosa lako, usiishi na hiyo hatia"

Baada ya hilo pambano na matukio yaliyotokea, sheria zikatungwa na kuubadilisha mchezo wa ngumi na kua tunavyouona leo.

Kwanza ikaamriwa ikitokea chochote kimegusa sakafu ya ulingo na siyo miguu ya bondia basi hiyo ni knockdown na itahesabiwa.

Ikaamriwa pia bondia akipigwa kwa KO leseni yake itafungiwa automatically kwa siku 45.

Badiliko kuu lilikua ni kupunguza raundi kutoka 15 mpaka 12. Utafiti ulionyesha mabondia wengi walipata majeraha au kuumia kuanzia raundi ya 13 na kuendelea.

Hili pambano lilibadilisha ubondia na likabadilisha maisha ya watu. Tukutane baadaye.

refa alijiua na uwaraza wake.
 
Ujue mashabiki wa boxing, wakiweza kuelewa tofauti kati ya boxer, swammer na slugger hawatapata shida ya kuelewa mchezo wa boxing.
Ewaa kuna ile natural style ya boxer halafu kuna ile anaona leo nakutana na mtu huyu inabidi niswitch. Mfano Pacquiao ni slugger ila kuna pambano utakuta anakua outboxer.
 
Ewaa kuna ile natural style ya boxer halafu kuna ile anaona leo nakutana na mtu huyu inabidi niswitch. Mfano Pacquiao ni slugger ila kuna pambano utakuta anakua outboxer.
Ila hakuna mashabiki wanafiki kama wa boxing [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]watakuwa na wewe ukiwa unashinda tu ukipigwa wanakukataa.

MF: Wilder akipigwa tena na Fury tarajia Wilder kupoteza zaidi ya 60% ya mashabiki wake kama AJ alivyopoteza mashabiki kwenye pambano la kwanza dhidhi ya Andy Ruiz.

MF : Tazama mvuto wa GGG ulivyopungua baada ya kupigwa na Canelo [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Back
Top Bottom