"Ray na Johari wana laana yangu na hawawezi kuiepuka"...Norah

"Ray na Johari wana laana yangu na hawawezi kuiepuka"...Norah

Money Stunna

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2011
Posts
13,053
Reaction score
6,304

BAADA ya hivi karibuni staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ kueleza mazito kuhusu Ray, Johari na Chuchu Hans, msanii mwenzake, Nuru Nassoro ‘Nora’ naye amefunguka kuwa laana ya walichomfanyia miaka ya nyuma itawatesa Ray na Johari mpaka kifo chao.

Akizungumza na GPL, Nora alisema Ray na Johari walimfanyia ‘mambo mabaya’ yaliyosababisha kupotea kabisa kwenye sanaa ya filamu hadi alipoibuka upya hivi karibuni.


“Kinachowasumbua Ray na Johari ni laana yangu na kweli nimeamini Mungu analipa hapahapa duniani kwani walinifanyia mambo ya ajabu, wakanipoteza kabisa kwenye fani, walinifanya nichanganyikiwe wakijua sitapona, lakini sasa hawaelewani tena wakati walikuwa wanapendana kama pete na kidole.

“Nakumbuka zamani nilikuwa nikishonea nywele nzuri lazima Ray naye akamnunulia Johari kama hizo za kwangu, alimtengeneza Johari akawa anaigiza kama mimi na kujifanya yeye ndiyo mimi mpaka waliponipoteza kwenye fani.


“Namshukuru Mungu nimejikongoja na hatimaye nimerudi tena kwenye sanaa, mabaya waliyokuwa wakinifanyia yamewarudia wenyewe, jamani mwacheni Mungu aitwe Mungu kwani nakesha nikiomba na ninaamini maadui zangu wote wataumbuka mchana kweupe,” alisema Nora.
-GPL
 
wabongo tunapenda maneno sijaona hata cha maana alichoongea
 
haituhusu! acha kuwa mdaku, ray na johar wanakuhusu nn? hata kama wanakuhusu ss yanatuhusu nn, kaongelee chumban na mkeo hachangie mawazo
 
Kajichubuuuuaaaaaa...halafu mbona km anataka kuvua nguo
 
walimpotezaje, kwa nyewele kufanana na za kwake tu??!!!
 
Back
Top Bottom