BADO sakata la kifo cha Steven Charles Kanumba The Great ni bichi na kwa mambo yalivyo, kuna uwezekano watu wengi zaidi wakaingia matatani kwa namna moja au nyingine.
Habari zinadai kuwa wakati upelelezi ukiendelea, kuna ambao tayari wamehojiwa na inawezekana wengi watahojiwa kwa kadiri ishu hiyo inavyozidi kuchukua sura mpya.
Ukimwondoa mtuhumiwa namba moja wa kifo hicho, Elizabeth Michael Lulu, ambaye alishahojiwa na kupandishwa kizimbani kisha kuwekwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Segerea, Dar, kuna wengine walio roho juu.
SETH BOSCO
Katika tukio hilo, pia tayari ndugu ambaye ni mdogo wa marehemu Kanumba, Seth Bosco naye alishafikishwa kwenye kituo cha polisi cha Oysterbay Kinondoni na kuhojiwa kuhusu anachokijua juu ya kifo hicho kwa kuwa ndiye mtu wa kwanza kuingia chumbani baada ya staa huyo kudondoka.
DAKTARI
Naye aliyekuwa daktari wa marehemu Kanumba aliyetajwa kwa jina moja ka Kabugi maarufu kama Kidume, alikuwa mmoja wa watu waliofika kituo cha polisi Oysterbay kutoa maelezo akiwemo mwigizaji swahiba wa marehemu Kanumba, Vincent Kigosi Ray.
Habari zinadai kuwa wakati upelelezi ukiendelea, kuna ambao tayari wamehojiwa na inawezekana wengi watahojiwa kwa kadiri ishu hiyo inavyozidi kuchukua sura mpya.
WALIOHOJIWA
LULUUkimwondoa mtuhumiwa namba moja wa kifo hicho, Elizabeth Michael Lulu, ambaye alishahojiwa na kupandishwa kizimbani kisha kuwekwa nyuma ya nondo za mahabusu ya Segerea, Dar, kuna wengine walio roho juu.