Raymond: Nikifuata misingi ya kazi baadhi ya watu wanafikiri ninaringa

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,969
14360167_1213814638693077_116105249617346560_n.jpg.pagespeed.ce.WIqUCRZtxG.jpg

“Kwa mfano, ninaweza nikawa misingi yangu ya kazi inaniambia baada ya show inabidi niingie kwenye gari niwahi hoteli. Shabiki anataka nishuke, nipige picha, aniombe namba ya simu,” Ray alimweleza Prince Ramalove wa Kings FM.
Anasema mara nyingi hayo ndio mambo aliyoelekezwa kufanya na uongozi unaomsimamia na ni muhimu kufuata.

“Huo ni msingi wa kazi, mtu hawezi kusema nimemdharau. Sometimes msingi wa kazi unaniambia haitakiwi nipokee simu ya interview ama simu ya promota akitaka show, anatakiwa apokee meneja, nitakavyomwambia ongea na meneja mtu ataona namdharau, lakini mimi nafuata msingi wa kazi, at end of the day siwezi kubadilika, nafuata msingi wa kazi sababu ndio unaonipa hela,” aliongeza.

Muimbaji huyo ametajwa kuwania tuzo za MTV MAMA katika kipengele cha Best Breakthrough Act.
 
afadhal umeliongoa hilo mana ulikua unanichanganya kweli
 
Rayvany siku hizi anaongelewa sana humu ndani kuliko yule ANAYEISHI KWA MAZA,KISHA NA YEYE ANAJIITA "KING"
Ukiendelea na tabia yako hii utakuja kufumuliwa marinda na marijal nakwambia
 
Rayvany siku hizi anaongelewa sana humu ndani kuliko yule ANAYEISHI KWA MAZA,KISHA NA YEYE ANAJIITA "KING"
Mkuu samahan labda nkueleze kitu usichokijua...ukienda tabata chama kama unaenda segerea uliza mtu yeyote anaeish mtaa ule kwa KING wap utaonesha ndo utakuja na maelezo mengine humu ndan.
.
.
.
Kyenekyaka mkighanile une
 
Duuh tabata chama?

mpaka tuanze kuuliza boda boda? mbona madale tunakwenda tuu
 
14360167_1213814638693077_116105249617346560_n.jpg.pagespeed.ce.WIqUCRZtxG.jpg

“Kwa mfano, ninaweza nikawa misingi yangu ya kazi inaniambia baada ya show inabidi niingie kwenye gari niwahi hoteli. Shabiki anataka nishuke, nipige picha, aniombe namba ya simu,” Ray alimweleza Prince Ramalove wa Kings FM.
Anasema mara nyingi hayo ndio mambo aliyoelekezwa kufanya na uongozi unaomsimamia na ni muhimu kufuata.

“Huo ni msingi wa kazi, mtu hawezi kusema nimemdharau. Sometimes msingi wa kazi unaniambia haitakiwi nipokee simu ya interview ama simu ya promota akitaka show, anatakiwa apokee meneja, nitakavyomwambia ongea na meneja mtu ataona namdharau, lakini mimi nafuata msingi wa kazi, at end of the day siwezi kubadilika, nafuata msingi wa kazi sababu ndio unaonipa hela,” aliongeza.

Muimbaji huyo ametajwa kuwania tuzo za MTV MAMA katika kipengele cha Best Breakthrough Act.
Mkuu tulia kwanza kabla ya kuleta uzi hebu angalia kuna makosa gani
 
Duuh tabata chama?

mpaka tuanze kuuliza boda boda? mbona madale tunakwenda tuu
Madale kwa dimondi ndo unaenda kwa bodaboda lakin nadhan kwa kiba hata kondacta ukimwambia nishushe kwa kiba anakushusha kabla ya kufika kituon chama ukitokea sanene ., then ckujua kama uliongea kwa ushabiki kama huo ila nilitaka kukueleza tu huyo jamaa ana kwake haraf pako pouwa sana tu ingawa hapafikii kwa huyo unaemshabikia

sawa basi nimekuelewa
 
Mkuu samahan labda nkueleze kitu usichokijua...ukienda tabata chama kama unaenda segerea uliza mtu yeyote anaeish mtaa ule kwa KING wap utaonesha ndo utakuja na maelezo mengine humu ndan.
.
.
.
Kyenekyaka mkighanile une
Kwahiyo King Crazy GK, kahama Upanga sasa yupo TBT ??
 
Back
Top Bottom