Raymond: Nilikata tamaa ya maisha

Raymond: Nilikata tamaa ya maisha

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Msanii wa muziki kutoka katika 'Label' ya WCB Wasafi Raymond amefunguka na kusema kuwa ilifika wakati alikata tamaa kabisa juu ya maisha hususani maisha ya muziki baada ya kusota kwa muda mrefu bila mafanikio.
Raymond%20_0.jpg

Msanii Raymond akifurahi baada ya kupewa zawadi ya gari aina ya Rav 4 na uongozi wake kwenye siku yake ya kuzaliwa jana Agosti 22, 2016

Raymond ameandika maneno haya wakati akitoa maneno ya pongezi na shukrani kwa uongozi wake mzima wa WCB Wasafi kutokana na namna walivyoweza kumbadilisha na kumpigania mpaka leo hii maisha yake yamebadilika na kufanya vizuri katika muziki ambao awali alishaukatia tamaa nao.

"Nimeamini Mungu hana upendeleo. Nilikuwa mtu nilie jikatia tamaa ndani ya miaka takribani minne, nilikuwa nikihangaika na muziki wangu lakini nakushukuru sana sana kaka lao Diamond Platnumz umenifundisha vitu vingi sana hadi leo naiona njia, Boss wangu Babu Tale ni mwaka wa tano sasa toka umenijua, umenivumilia kwa mengi hadi leo hii haujanichoka na unanisaidia kwa moyo mmoja". Aliandika Raymond

Mbali na hilo Raymond aliendelea kutoa shukrani kwa viongozi wake wengine huku akisema kwa mafanikio aliyopata sasa anaamini Madee anafurahia maana anajua jinsi gani ambavyo amehangaika na muziki.

"Asante sana Boss Sallam Sk kwakupigania kila siku thamani ya muziki wangu, nakuakikisha nafika sehemu nzuri Mkubwa Fella wewe ni zaidi ya mzazi maana umenilea nakunifundisha mengi kwenye muziki. Made Ali sitoacha kukushukuru kaka lao wewe ni kioo naamini unafurahi kuniona mdogo wako hapa nilipo maana unanijua sana". Aliongeza Raymond

SOURCE; EATV NEWS
 
madee & diamond[emoji108][emoji122][emoji122][emoji122]
babutale [emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26][emoji26]
 
Hivi wasanii wa WCB accounts zao za youtube wanalipwa direct au kuna ujanja ujanja?
Naskia sikuhiz ni direct pia kuna kampuni bongo zinasimamia videos za wasanii Youtube na mpunga unatoka google direct fedha zinaenda kwa msanii no longolongo.
According to KingKapita dogo flani alikua anaimba nae akaenda nje kusoma IT karudi bongo ndio wanamiliki hyo kampuni alihojiwa na Bongo5
 
Mkuu google hawalipi mtu akiwa na page YouTube isipokuwa mtu kama anapage YouTube na anapata views nyingi anaweza kupata dili la kuweka video yenye tangazo la biashara na malipo atapewa na huyo aliemtangazia biashara google hausiki!

Msome Bunsenburner hapo juu
wewe hujui kitu.......
 
Naskia sikuhiz ni direct pia kuna kampuni bongo zinasimamia videos za wasanii Youtube na mpunga unatoka google direct fedha zinaenda kwa msanii no longolongo.
According to KingKapita dogo flani alikua anaimba nae akaenda nje kusoma IT karudi bongo ndio wanamiliki hyo kampuni alihojiwa na Bongo5

Mkuu ukipata jina la hiyo kampuni tutajie
wanalipa sio tu wanamuziki
anyone mwnye views nyingi
 
Yes google wanalipa ukipata views nyingi..
a lot of money
Kimsingi Google hawalipi kutokana na views as views bali views for ads/matangazo! The problem, thamani ya haya matangazo yanatofautiana kutoka nchi moja hadi nyingine for a very known reason! Kwa mfano, views za US na Europe zina thamani kubwa kuliko za Afrika! Za South Africa zina thamani kubwa kuliko za Tanzania! Hata hivyo, inategemea na target audience. Kama kinachotangazwa ni iPhone 7 na target audience ni Europe & Africa; single click from Europe viewer itakuwa na thamani maradufu compared na single click ya viewer from Africa.
 
Back
Top Bottom