joseph1989
JF-Expert Member
- May 4, 2014
- 17,420
- 35,765
Mbona kipindi kile Rockstar mmoja wa madirector akiwa Kiba waliichukua YouTube account ya Barakha Da Prince, mbona hamkuongea humu ,mkaishia kusema "dogo ana dharau" ila huku WCB mnasema "wanaonewa".hujui unachokiongea unaweka ushabiki mbele hivi unajua nyimbo zao wanzotoa wakiwa WCB zote sio mali yao, unajua mpaka hizo account zao za social media sio mali, wao ni kama wafanyakazi wengi pale kitu ambacho ni tatizo kwenye sekta ya sanaa na ubunifu. rejea kesi ya konde na rich mavocal, konde alisaidiwa na jembe ni jembe lakini wapi ruch mavoko.
sikatai hata ulaya hayo mambo yapo mfano TLC yalishawakuta hayo walikua wanaingiza mpunga mwingi ila wao waliishia kununuliwa magari, nguo na pesa kidogo ya matanuzi lakini badae wastuka wakaenda mahakamani kudai haki zao sema badae wakapotea baada ya left eye kufa
Ila kama hujui kwa Nigeria baadhi ya Label si YouTube mpaka jina unalotumia ni mali ya Label ukiondoka jina unabadilisha mf Kiss Daniel baada ya kutoka kwenye label anajiita Kizz Daniel na YouTube yake wameichukua.
Mayorkun pamoja na ukubwa wake nyimbo zote zipo chini ya boss wake Davido na nyingi zipo kwenye account ya Davido hata youtube si mali yake Mayorkun, Wizkid mwenyewe alikuwa chini ya Bank W ,baada mkataba kuisha YouTube ikabaki kuwa mali ya label.Hata Wizkid,YouTube account za wasanii wake zipo chini ya label yake ya Starboy.
Jembe ni Jembe hakumsaidia Konde bali aliona potential ya Konde kibiashara na ndio maana akatoa hela yake, leo hii Konde akivunja mkataba lazima alimpe Jembe ni Jembe na msanii yoyote akitoka Konde lazima awalipe Konde Gang sababu waliwekeza hela yao kwao,JembeniJembe si boya yule mtoto mjini na ana Phd anajua hela aliyo itoa LAZIMA irudi.