Rayvanny kaambiwa alipe milioni 500 aondoke WCB

Rayvanny kaambiwa alipe milioni 500 aondoke WCB

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Mtangazaji mkongwe wa mambo ya showbiz na udaku Tanzania, Maimartha amezungumzia juu ya taarifa za Rayvanny kuoma kuondoka katika lebo ya WCB.

Haya ndiyo maneno yake aliyoyasema wakati akihojiwa na BONGO TRENDY TV:

“Habari zao ninavyojua ni kuwa Rayvanny aliomba kutoka WCB, akaambiwa atoe milioni kadhaa, kwa hiyo katika kujiandaa kama ilivyokuwa kwa Harmonize naye aliambiwa milioni 500, ukiona mwenzako ananyolewa zako tia maji.

“Ukiangalia Wasafi wanachokidai ni sawa jamani, sema tu negotiation iwe ya busara, hata hao wengine nao wakitaka kutoka wajiandae, hao kina Mbosso,” anasema Maimartha.
 
watanzania wengi ni masikini na wanauoga hizi zama wengi tumeanza kusikia million 500 n unyonyaji kwa sababu ndio mziki unakua na nchi kukua ila huko mbeleni hii pesa na kwa kazi waliyofanya wasafi wajukuu na watoto watawashanga sana.

bado kazi zinaenda kindugu sana.

kwa views za youtube
channel yake ya youtube,boomplay,audio mack,matangazo, wadhamin na itune hizo pesa zinarudi akilipia.

bado brand aliyotengenezwa hio pesa haitoshi kabisa.

nikisema haitoshi namaanisha show atakazo piga ndani ya miaka 5.
wadhamini wanaweza kumpa hyo hela akalipa.

watz n wajinga, kwa nini wasanii wakitoka kwa kiba hamuwazi ?

investment ya kuwatengeneza wasanii ni kubwa.

hembu fikilia kuhusu Zuchu ukubwa alionao ndani ya muda mfupi unafikili vdeo,mavazi ni bure na kshoot vdeo.

brand ya wasafi inawapa vitu vya pekee wasanii wanao pita pale.

harmonize sikuwahi kumjua.
rayvanny nilimjua ila si kwa huu ukubwa.
mbosso nilimjua ila amefit sana.
zuchu ckumjua bora nandy.

na kuna mwingine ambae tutakua hatumjui watakuja kutake over sana.

wanaperfom afrima, show za mtv , dubai hivi sfr zote hizo kbl hajajulkana mnahisi ni bure au waliweza kuenda.

mtu tu ukiambiwa toa nauli ya kwenda kigoma ukiwa dsm unatoa macho,mtu anabeba clue nzima tour nzma .

kwanza hata wakichukua hiyo hela wasanii wanao onyesha ukubwa ni wale waliopita wcb hakuna label yenye uwezo km wcb.

kwa hio pesa asiwe na kinyongo kabisa atoe.

watu tunakaa na ndugu zetu miaka hakupi mtaji sembuse mtu ambae hakujui ana invest hivyo hlf hakunji kuondoka mbona mnapenda vya bure wabongo na kulalamika hovyo.
 
Milion 500 fair sana...!! Alaf hii ni chai , inakuwaje ubuyu kama huu unampita , Mange na Karl mastory uje uangukie Kwa maimartha
 
Hio hela ray hana. Harmo mwenyewe mpaka akasaidiwa na mzungu
 
Hapo atafute wateja auze brand yake ya Next level Music apate hela
 
Mtangazaji mkongwe wa mambo ya showbiz na udaku Tanzania, Maimartha amezungumzia juu ya taarifa za Rayvanny kuoma kuondoka katika lebo ya WCB.

Haya ndiyo maneno yake aliyoyasema wakati akihojiwa na BONGO TRENDY TV:

“Habari zao ninavyojua ni kuwa Rayvanny aliomba kutoka WCB, akaambiwa atoe milioni kadhaa, kwa hiyo katika kujiandaa kama ilivyokuwa kwa Harmonize naye aliambiwa milioni 500, ukiona mwenzako ananyolewa zako tia maji.

“Ukiangalia Wasafi wanachokidai ni sawa jamani, sema tu negotiation iwe ya busara, hata hao wengine nao wakitaka kutoka wajiandae, hao kina Mbosso,” anasema Maimartha.
Mwacheni jamaa yangu. Nyie si mpambanie tu maisha yenu?
IMAG3266.jpg
 
Back
Top Bottom