RAYVANNY KASHUKA NA KUISHIWA MBINU KIMUZIKI

RAYVANNY KASHUKA NA KUISHIWA MBINU KIMUZIKI

B M F ICONIC

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
824
Reaction score
1,631
Moja kwa moja kwenye mada.

Kumekuwa na mijadala mitandaoni kua Rayvany anaimba nyimbo zake kwa mfumo/mtindo uleule kitu ambacho kinasababisha watu kutomuelewa msanii huyo
Mfano hio post ya X
Screenshot_20241023-151450_VidMate.jpg

Mfano.
Nyimbo kama Teamo, Number one ft zuchu, I miss U ft zuchu. Mfumo wa uimbaji na Beat ni uleule wa kufanana. Kitu ambacho kina fanya mashabiki wa muziki kutomuelewa msanii huyo.

Msanii Madee pia asha toa malalamiko hayahaya kupitia kwa babu tale afikishe ujumbe kwa msanii huyo

Ikumbukwe kabla ya Rayvanny kujiunga WCB alikuwa Rapper chini ya TipTop connection iliokuwa inasimamiwa na Madee. Japo Rayvanny ana uwezo wa ku freestyle automatic bila kuandika tumeuoona uwezo wake wa kuchana kwenye Super nyota mbeya.

Lakini ameshindwa kuwapa mashabiki wa muziki vitu tofauti hali inayofanya kumchukulia kua hana maaajabu mziki wake ni uleule

Rayvanny ashaeleza moja ya malengo yake kimuziki ni kusikika na ku li win soko la kimataifa yaani worldwide na kuhakikisha kazi zake zinatazamwa na kupata engagement nje ya mipakya Tanzania.
Mfano hapo chini
Screenshot_20241028-132717_TikTok.jpg

Nguvu nyingi kaziamishia kwenye Soko la kimataifa ili kujulikana pande hizo.

Kama tunavyomuona akishirikiana na wasanii wa nchi tofauti kama Nora fatehi wa India, Maluma( carebean), Gerison Insrael wa Angola/ portugal, Luana vjoalica wa Albania n.k Nii kweli anatuwakilisha vizur na mipango yake inaenda vizuri kimataifa.
Pia ndo msanii alie vizuri kwa lugha na anaeweza kuimba kwa kiingereza Fluently.

Changamoto ni kufanana midundo/ idea/maudhui/Beat katika nyimbo zake.

Nawasilisha.... Leta maoni yako
 
Back
Top Bottom