Rayvanny + MacVoice = Nyota ya upepo + Nyota ya moto

Rayvanny + MacVoice = Nyota ya upepo + Nyota ya moto

Unajipa moyo tu nyota ya mtu unaitazama vp? Ungetwambia wamezaliwa miezi ipi? (Nafahamu nyota husomwa kwa majira ya kuzaliwa) kama si hivyo bas ni mambo mengine we umetizama nini?

Kweli upepo huendana na moto kama ilivyo maji kwa udongo ila kwa Hawa kuna ujinga mwingi (usiniulize hata Mimi siujui)
Nyota zipo nne tu mkuu...Upepo, Maji, Moto na Udongo....hizo za wazungu sijui miezi ya kuzaliwa ni magilini tu hazi-work kwenye ulimwengu wa mafanikio.
 
Nyota zipo nne tu mkuu...Upepo, Maji, Moto na Udongo....hizo za wazungu sijui miezi ya kuzaliwa ni magilini tu hazi-work kwenye ulimwengu wa mafanikio.
Hahaha nyota 4 hahaha kumbe bado ujajua usemacho
 
Nimetoka kuchungulia kwenye ulimwengu halisia unaoiendesha dunia...nimekuta Rayvanny ana nyota ya upepo.. nafikiri wote mnafahamu nguvu ya upepo ni invisible ila ukipuliza unaweza kupeperusha mpaka milima. Nyota ya upepo ni pumzi, upepo ni safari ukiwa kwenye maji.

Nimemtazama msanii wake mpya kwenye rekodi label ya nextlevel anaeitwa MacVoice. Nimekuta MacVoice ana nyota ya moto...wote tunajua balaa la moto...moto una angaza, ila ukicheza nao unaungua.

Sasa ni kama coincidence upepo umekutana na moto.... Rayvanny kumtoa MacVoice ni kama upepo mkali kupuliza moto... cheche zitaruka, mwangaza utawaka kila pande na ataesogea kujaribu kuzima moto ataungua abakie majivu.

Hii combination yao kwenye kizazi hiki za muziki ni Mungu tu anaejua balaa lao... Tutegemee kuona maajabu na mapinduzi kwenye sanaa ya bongofleva.

Wale haters nawataadhalisha kaeni mbali na nextlevel mtabaki majivu.
Let's wait and see.
 
Back
Top Bottom