Rayvanny: Nimetumbuiza World Cup, FIFA wakam-follow Diamond

Rayvanny: Nimetumbuiza World Cup, FIFA wakam-follow Diamond

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Rayvanny, amezungumzia umuhimu wa wasanii wa Tanzania kushiriki katika majukwaa makubwa ya kimataifa, akieleza kuwa hatua hiyo inachangia kukuza tasnia ya muziki nchini pamoja na kufungua milango ya fursa kwa wasanii wengine.

Rayvanny amesema mafanikio ya wasanii wachache kufika na kutumbuiza kwenye majukwaa hayo makubwa yanaifanya dunia kuitazama Tanzania kwa jicho tofauti, jambo linaloongeza nafasi kwa vipaji vingine kuonekana na kuthaminiwa kimataifa.

Ametolea mfano wa tukio la hivi karibuni ambapo Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) wamemfollow msanii Diamond Platnumz kwenye mitandao ya kijamii, katika kipindi hiki alichotumbuiza kwenye jukwaa la Countdown Concert kuelekea mashindano ya Kombe la Dunia.

Soma: Msanii mliyesema kaishiwa, Rayvanny kashachaguliwa huko kutumbuiza kwenye Kombe La Dunia

Hata hivyo, Rayvanny amesisitiza kuwa FIFA Kumfollow Diamond Platnumz hakuhusiani na yeye bali ni matokeo ya juhudi na mafanikio ya Diamond Platnumz mwenyewe katika kuiwakilisha vyema Tanzania kwenye jukwaa la kimataifa.

 
Back
Top Bottom