Rayvanny; Nitaondoka WASAFI (WCB) kwa amani

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,393
Reaction score
3,237
Msanii Raymond Shaban Mwakyusa AKA Rayvanny aliyepo chini ya label ya Wasafi Classic Baby (WCB) amesema atahakikisha anatoka kwenye label hiyo kwa amani. Katika kipindi cha Salama Na Rayvanny kinachorushwa EATV aliulizwa na Salama kuwa wapo watu wanasema Rayvanny ndiye anayefuata kuondoka WCB baada ya Harmonize, Rayvanny alisema jambo hilo linawezekana, na wanaosema hayo wanaongea kwa kuwa yeye ni msanii anayefanya vizuri WCB. Rayvanny alisema Kama ukifika wakati wa yeye kuondoka WCB basi atahakikisha anaondoka kwa amani bila migogoro yoyote.

NINA TABIA NJEMA
Katika mambo mengine aliyosema Rayvanny ni kwamba yeye hanywi pombe, havuti sigara wala bangi hata hivyo alikataa kutaja starehe anayoipenda. Amedai yeye ni mtu anayemtegemea na kumwamini Mungu na kwamba mama yake ni mlokole wa dhehebu la Baptist huko mkoani Mbeya ambapo pia amedai yeye alikuwa akiimba kwaya kanisani. Anasema hajawahi kwenda kwa mganga na haamini katika kutegemea nguvu za giza.

MSISHANGAE SIKU NIKIIMBA GOSPEL

Katika kuthibitisha ucha Mungu Rayvanny amesema watu wasijekushangaa siku akiacha bongo flavor na kuhamia kwenye muziki wa injili.

SIPO SINGLE

Pamoja na kukataa kumtaja anayedate naye Rayvanny amesema kwa sasa hayupo single.

Pia soma;

Thread 'Rayvanny aaga rasmi WCB- Wasafi, ashukuru kwa fursa aliyopewa ya kuwa mwanafamilia wa Wasafi' Rayvanny aaga rasmi WCB- Wasafi, ashukuru kwa fursa aliyopewa ya kuwa mwanafamilia wa Wasafi
 
Kuondoka Wasafi hakujawahi kuwa kwa amani. Waswahili tunajuana.

Ondoka uone kama hata Wasafi media watakuja kukuletea hata Mic ya interview.

Waswahili hata tukitongoza demu akikataa tunakunja, ni beef dadeki.

Anyway, huo uwezo wa kuondoka huna na hata kama ukijitutumua kuondoka humalizi 2 months utakuwa umeshabuma.

Kuwa mwaminifu hapo upate japo kodi ya nyumba.

Mr. T Touch naye alijifanya anaondoka kwa Nay wa Mitego kwa amani, lakini Nay alikunja.
 
Kiukweli wasanii ambao diamond alibahatisha ni Kondeboy , ray vanny na Zuchu , Mboso still anasua sua japo ni afadhali , lava lava ni gharasa , qeen darling ndo usiseme😀😀
Nafikiri Uwanja wa muziki ungekuwa huru with free Promoters and media, hapo ndio label zingekuna vichwa kutafuta vipaji.

Kwa mfumo wa shows uliopo ndio maana unawaona kina Gig money na Nai majukwaani. Sasa hao kina Mbosso na Lavalava ni bora mara 100 kuliko hao.
 
Hawezi kusema ila moyoni Dogo anaumia sana, Mkataba wake na Wcb ni unyonyaji wa hali ya juu 70% yote ni ya Boss yeye anabakiwa na 30%
Ok pamoja na kunyonywa huko ni wasanii gani wanamfikia kimaisha na kimafanikio? Wewe binafsi unamfikia? Mavoko aliekua ananyonywa wcb akaamua kutonyonywa yuko wapi saizi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…