RC Chacha aahidi milioni 50 kwa Tabora United ikiilaza Simba SC

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wakuu

Mmesikia huko?

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, ameahidi kitita cha shilingi milioni 50 kwa timu ya Tabora United iwapo itaibuka na ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wao ujao. Chacha alitoa ahadi hiyo leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete, wakati wa zoezi la kuchangia damu, tukio lililofanyika kusherehekea ushindi wa Tabora United dhidi ya Yanga.

Pia, Soma: RC wa Tabora, Paul Chacha awakabidhi wachezaji wa Tabora United Tsh. Milioni 50 kwa kusalia katika Ligi Kuu

"Siku wakimdondosha yule mnyama mkubwa yule…milioni 50 itawahusu” maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha akitoa ahadi ya kitita cha fedha kwa Tabora United, kama itaifunga Simba watakapokutana."

"Chacha ametoa ahadi hiyo leo katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora, Kitete wakati akizungumza kwenye zoezi la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea ushindi wa Tabora United dhidi ya Yanga."

"Sherehe hizo zimefikia tamati leo na tangu timu hiyo ipate ushindi, wadau na mashabiki wa Tabora United wamekuwa katika furaha karibu wiki nzima."
 
Atakuwa Yanga huyu...

Kama ana nia njema awape kwanza 50ml za kuwafunga wachawi.
 
Naona ànawàkatià tiketi ya kushuka daraja. Huwezi kufanya sherehe wiki nzima kisa kuifunga utopolo na ukabaki salama.
 
Back
Top Bottom