RC Chacha aahidi milioni 50 kwa Tabora United ikiilaza Simba SC

Huyo a
Wakuu

Mmesikia huko?

Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha, ameahidi kitita cha shilingi milioni 50 kwa timu ya Tabora United iwapo itaibuka na ushindi dhidi ya Simba katika mchezo wao ujao. Chacha alitoa ahadi hiyo leo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora, Kitete, wakati wa zoezi la kuchangia damu, tukio lililofanyika kusherehekea ushindi wa Tabora United dhidi ya Yanga.

Pia, Soma: RC wa Tabora, Paul Chacha awakabidhi wachezaji wa Tabora United Tsh. Milioni 50 kwa kusalia katika Ligi Kuu

"Siku wakimdondosha yule mnyama mkubwa yule…milioni 50 itawahusu” maneno ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha akitoa ahadi ya kitita cha fedha kwa Tabora United, kama itaifunga Simba watakapokutana."

"Chacha ametoa ahadi hiyo leo katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora, Kitete wakati akizungumza kwenye zoezi la kuchangia damu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea ushindi wa Tabora United dhidi ya Yanga."

"Sherehe hizo zimefikia tamati leo na tangu timu hiyo ipate ushindi, wadau na mashabiki wa Tabora United wamekuwa katika furaha karibu wiki nzima."
ameharibu, sasa simba itawachapa zaidi ya bao 6. Angeongea kimya kimya
 
Hela hizi zinatoka kwa nani?
 
Tabora united wakilewa sifa siku hiyo wataoga magoli sisi(simba) sio kama wale(elewa neno wale)
 
Hawawezi kuifunga Simba. Hata Yanga waliwaweza kwakuwa kina 🗝️ waliamkia kwenye shisha.
 
Mpira ni uchumi , ajira na biashara, Tabora United ikiwa tishio uchumi wa Tabora utakua mkubwa na huko kutachangamka, hivyo kutoa ahadi kama hizo ni sawa, japo huyu big boss atakuwa mwananchi tu, mbona mnyama kamuwekea bond kubwa achinjwe na kisu butu!!
kama huna D mbili huwezi kumuelewa.
 
HAPO NDIO UJUE NCHI INA VIONGOZI WA HOVYO.

NILITEGEMEE ATOE AHADI TIMU YAKE IKICHUKUA UBINGWA YEYE ANAWAZA KUZIFUNGA SIMBA NA YANGA.

ZEZETA.
 
Back
Top Bottom