Pre GE2025 RC Chalamila akutana na Waandamanaji wa CHADEMA. Awatakia heri kwenye maandamano na kuwasihi kufikisha ujumbe walipokusudia

Pre GE2025 RC Chalamila akutana na Waandamanaji wa CHADEMA. Awatakia heri kwenye maandamano na kuwasihi kufikisha ujumbe walipokusudia

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewatakia kila la heri wafuasi wa CHADEMA waliokutana maeneo ya Mbezi Mwisho stendi ya Magufuli kwa ajili ya kuanza maandamano ya amani na kuwataka kuulinda uwekezaji uliopo ndani ya Jiji hilo wasiuharibu na badala yake wafikishe ujumbe walioukusudia siku ya leo.

"Mnatakiwa kufikisha ujumbe pale mlipokusudia, serikali tuko na nyie na tunawatakia kila la heri, ninyi na mimi ni wana Dar es Salaam penye mzunguko mkubwa wa pesa, penye hospitali kubwa na uwekezaji mkubwa, maandamano yetu yanapaswa kulinda uwekezaji wote huo, Rais Samia na viongozi wote wamesema wacha watu waandamane," amesema Chalamila

View attachment 2881134
Kwani inagharimu kitu gani kuwa muungwana kiasi hiki?
Siku zote huwa nasema hii nchi watu wake hawajaamua tu kuwa serious sababu ya maujinga mengi waliyo nayo. Siku wakiachana na hayo maujinga ujinga nchi itaruka ghafla na kufika mbali sana.
Yaani watu wanaishi wakiaminishana eti U-CHADEMA au U-CCM wake ndiyo tatizo kubwa kwenye nchi hii?
 
Hawana kazi za kufanya hao nyumbu wa Chadema.

Makonda anasema Samia ni mama vinginevyo ingekuwa awamu ya chuma angewafyeka wote [emoji23][emoji23]
Ila nyie fisi mnaosombwa na malori kama mchanga kwenda kwenye mikutano ya Makonda ndio mna kazi za kufanya?
 
Hawana kazi za kufanya hao nyumbu wa Chadema.

Makonda anasema Samia ni mama vinginevyo ingekuwa awamu ya chuma angewafyeka wote 😂😂
Kwa mnasifia kiongozi dikteta kuua wananchi wake In cold blood? CCM ni hatari kwa mstakabali wa Amani ya taifa hili 🤔
 
Back
Top Bottom