Habari JF , leo katika pitapita zangu nimekutana na kauli iliyozua maswali mengi sana kutoka kwa RC Chalamila , kwa ataeshindwa kununua gloves akajifungulie nyumbani .
Kimsingi inawezekana ni kauli sahihi katika mambo mengine ya afya lakini katika suala la uzazi ambalo lina faida kwa Serikali na familia inaweza isiwe sahihi kwa sababu :-
1.Kiafya ,Kijamii na kisiasa Mama mjamzito ni mtu anayehitaji mahitaji na huduma maalumu .
2.Elfu hamsini sio hela ndogo , Watanzania wengi sana wanafanya kazi wanapata hela ambayo inaishia mahitaji ya kula , Mavazi na kulala ukiwa muajiriwa unaweza usiliewe hili lakini ndiyo hali halisi ya mtaani. Hata watu wanaotumia Bima ukiwastukiza walipe hata 2500 kwa Ajili ya kipimo au dawa katika 100 watakao mudu ni kama 10 tu
3.Afya ya Uzazi Msingi wa Uchumi na Maendeleo ya Nchi yoyote ile ,Nchi nyingi sana sasa hivi zinapambana kuongeza Raia , hivyo ni suala la kiserikali kwa asilimia kubwa . Katika hili suala Serikali inaweza fanya yafuatayo
Mwisho Kauli na maelezo ya RC Chalamila iamshe jamii kujipanga vizuri pindi inapopata mama mjamzito.

>>Kiafya kutokana na mabadiliko yanayotokana na ujauzito Changamoto nyingi sana zinaweza mkuta huyu mama ikiwemo kupoteza mtoto , mama mwenyewe au wote au kumuachia mama kilema/ugonjwa maishani .Hivyo kuna umuhimu Serikali kuweka mkono wake kwa kusaidiana na familia.
>>Kwenye jamii mama mjamzito amepewa hadhi ya peke yake ukiwa mahospitalini ,maofisoni hata kwenye vyombo vya usafiri utaliona hili , Hivyo kutoa kauli ya kutojali ya kujifungulia Nyumbani ukikosa gloves ni kugombana na Jamii .
>>Kisiasa Mama mjamzito ni Mali ya Serikali na taarifa zake zote lazima zihifadhiwe na kufuatiliwa kwa upekee ,Hapa Nguvu kazi inatengenezwa watu wakipunguza kuzaliana itakuwa shida ndio maana hata Serikali suala la uzazi limepewa kipaumbele.
2.Elfu hamsini sio hela ndogo , Watanzania wengi sana wanafanya kazi wanapata hela ambayo inaishia mahitaji ya kula , Mavazi na kulala ukiwa muajiriwa unaweza usiliewe hili lakini ndiyo hali halisi ya mtaani. Hata watu wanaotumia Bima ukiwastukiza walipe hata 2500 kwa Ajili ya kipimo au dawa katika 100 watakao mudu ni kama 10 tu
3.Afya ya Uzazi Msingi wa Uchumi na Maendeleo ya Nchi yoyote ile ,Nchi nyingi sana sasa hivi zinapambana kuongeza Raia , hivyo ni suala la kiserikali kwa asilimia kubwa . Katika hili suala Serikali inaweza fanya yafuatayo
>Kuhakikisha huduma za uzazi zinapatikana muda wote bure au kwa bei nafuu , kuwepo na taarifa maalumu ni vitu gani vitachangiwa na Serikali na vipi Mama mjamzito au
>Kuwepo Bima ya Uzazi ambayo itakuwa ya bei ya chini sana na itatumika kipindi cha ujauzito/uzazi .