Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huyo RC, amekuwa mkweli, tofauti na wengine ambao miradi mingi inayotekelezwa na taasisi za majeshi, kusua sua, na viongozi kuogopa kuwatimua kwenye kazi tofauti na wakandarasi wengine. Tatizo liko hapa ofisi nyingi za halimashauri zinajengwa chini ya tamisemi, hawatoi pesa kulingana na awamu za ujenzi, hivyo mkandarasi anashindwa kuendelea na kazi, na kama ingekuwa ni kampuni binafsi wanatishwa wanakopa pesa sehemu nyingine ili mradi uende tu, ila kama ni jwtz, pesa watatoa wapi?!! Mala ngapi jiwe ametoa maelekezo kwwnye taasisi ya TBA, kuwa wanakwamisha miradi kuisha kwa wakati?? Tatizo jingine kwenye gharama za ujenzi, wanatoa gharama ndogo kutafuta sifa, ila kazi ikianza tu ndio balaa, pesa hazitoshi kulingana na gharama halisi za ujenzi!! Yale maghorofa ya magomeni toka wapewe muda wa mwisho magereza, umefikia wapi?? Ma RC, DED, DC, wana kazi sana kwenye miradi inayosimamiwa na taasisi hizi, bora hata huyu amethubutu. Kwa mfumo wa sasa hakuna pesa ya kujenga jengo la halimashauri inayotoka halimashauri.Chalamila ni kiumbe mjanja mjanja sana! Isije ikawa ameshatafuta mzabuni mwingine ili ale 10% ya faster faster! Maana huu ni mwaka wa uchaguzi.
Maamuzi yanaonekana ni ya kukurupuka kabisa. Yaani Msimamizi ameeleza wazi ya kwamba Halmashauri imekua ikitoa fedha za ujenzi kwa kusua sua! Badala ya kumkomalia DED atoe hela za ujenzi kwa wakati, yeye anaamua kuwadhalilisha Wanajeshi wetu!!
16 Jun 2015 · Mzinga Corporation is a Government Institution under the Ministry of Defence. The Corporation's Head Office is in Mzinga, Pwani.