RC Chalamila awataka wakazi wa DSM wajilinde Wao na familia zao dhidi ya matukio hatarishi badala ya kuwatupia Polisi lawama

Mkuu wa mkoa wa DSM Albert Chalamila amewataka wananchi wa DSM kujilinda wao na familia zao dhidi ya matukio yoyote yanayoweza kuhatarisha Amani na Usalama wao

RC Chalamila amesema SI HAKI kuwatupia lawama Polisi kwa kila Jambo.
---
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewataka Wakazi wa Dar es salaam kutambua umuhimu wa kujilinda na kuzilinda Familia zao dhidi ya matukio yoyote yanayoweza kuhatarisha amani na usalama wao badala ya kuwatupia lawama Polisi kwa kila jambo.

RC Chalamila amesema hayo wakati akifanya ziara ya kukagua Zahanati ya Kurasini Wilayani Temeke leo September 27,2024 “Leo kwenye mkutano nitaongea baadhi ya vitu ambavyo Watu wanalalamikia utekaji sijui nini, leo kwenye mkutano nitawapa data namna Vijana wetu tuliowazaa wanavyoshiriki kwenye baadhi ya matukio, nitawapa tukio la Mama ameuawa na kuchinjwa vipande karibu 30, wa hapahapa Temeke Mbagala na aliyefanya na nitawaeleza alifanyaje”

“Nitawapa matukio ya Watu wameenda kwa Waganga wa kienyeji, Mganga ameona wana hela akawanywesha sumu wakafa akaiba hela akawazika bila taarifa, leo mnapokuta kuna matukio Watu wanasema Polisi ndio wanateka, Vyombo vya Dola vinateka, kuna vitu mnakosa uelewa na kwasababu mnakuja kwa mihemko hamuwezi kujibiwa kistaarabu hata kidogo”

"Halafu kwa mashinikizo mnasema tunataka kuingia barabarani, lazima Serikali iseme, kama tunataka kujenga Taifa letu ni vizuri tujenge mijadala ya kuulizana maswali, kuna vitu vinafanyika kama sanaa kuna vingine kweli Watu wamefanya, ebu niwaulize Baba na Mama wamefunga mlango wamekwenda ndani kulala asubuhi unaambiwa uko ndani Watu wameuana hivi niambieni kwenye mazingira hayo Polisi wanahusikaje?

kwahiyo Polisi awaambie laleni Mimi nipo mlangoni mpaka kunakucha inawezekana jamani?, kwahiyo Mlinzi wa kwanza kwa kila jambo ni Mwananchi mwenyewe”

“Hata Mimi Mkuu wa Mkoa unaweza kukuta hapa nalindwa lakini hawa wanaonilinda nakuwa nao nyumbani?, kama Mimi nitaondoka kwangu na Mkuu wa Wilaya tunakwenda huko Mbagala kunywa pombe tukishakunywa pombe tunachukua Wake za Watu halafu nasema watatufanya nini, watatupiga makofi huko na watanichinja, kwahiyo ulinzi wa kwanza ni wewe mwenyewe Raia”

“Mtu unazaa Mtoto huelewi ameenda wapi kutoka asubuhi hadi jioni, inafika saa mbili ndio unasema mtafuteni Mtoto, hivi kweli Mtoto huyo alikaa kwenye tumbo lako au la jirani?”

Pia soma
- RC Chalamila: Matukio ya Mauaji na Utekaji Watoto yapo lakini siyo kama yanavyoripitiwa, mengi siyo ya kweli

Source: Ayo TV
Huyu naye ana akili kibaba!!

Hivi nani aliwahi kuwashutumu polisi kwa vifo vilivyotokea ndani ya nyumba za watu? Naona Dar tuna RC ambaye ama hazimtoshi kichwani au unafiki umemwondolea akili.

Polisi wanalalamikiwa kwa utekaji kwa sababu ni polisi waliwaita vituoni, halafu watu hao hawakurudi tena. Wengine baada ya kutekwa walipumzishwa ndani ya vituo vya polisi, kisha wakapotezwa. Wengine walichukuliwa mbele ya macho ya watu wengi, mbele ya polisi, watekaji wakajitambulisha kuwa ni polisi , wakiwa na smg na magari yasiyo na namba (ambayo huwa wanapenda kutumia agents wa serikali), halafu huyu punguani anakuja na mifano ya mambo yasiyoendana kabisa na matukio!! Hopless RC!!
 
kuna vyama wanatoa kafara na kuwachukua misukule wanachama wao 🐒
Wewe nawe ni shetani punguani. Yaani wapinzani wamteke mtu wampeleke kwanza kituo cha polisi, halafu wakampoteze!! Wewe damu za watu zimekupotezea hata ile reasoning ndogo kabisa.

Ninyi wauaji mliopo humu JF mnafamaika.
 
Wewe nawe ni shetani punguani. Yaani wapinzani wamteke mtu wampeleke kwanza kituo cha polisi, halafu wakampoteze!! Wewe damu za eatu zimekupotezea hata ile reasoning ndogo kabisa.

Ninyi wauaji mliopo humu JF mnafamaika.
kwanini vijana wa watu wanafanywa misukule lakini dah?🤭
 
Mkuu wa mkoa wa DSM Albert Chalamila amewataka wananchi wa DSM kujilinda wao na familia zao dhidi ya matukio yoyote yanayoweza kuhatarisha Amani na Usalama wao

RC Chalamila amesema SI HAKI kuwatupia lawama Polisi kwa kila Jambo.
---
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewataka Wakazi wa Dar es salaam kutambua umuhimu wa kujilinda na kuzilinda Familia zao dhidi ya matukio yoyote yanayoweza kuhatarisha amani na usalama wao badala ya kuwatupia lawama Polisi kwa kila jambo.

RC Chalamila amesema hayo wakati akifanya ziara ya kukagua Zahanati ya Kurasini Wilayani Temeke leo September 27,2024 “Leo kwenye mkutano nitaongea baadhi ya vitu ambavyo Watu wanalalamikia utekaji sijui nini, leo kwenye mkutano nitawapa data namna Vijana wetu tuliowazaa wanavyoshiriki kwenye baadhi ya matukio, nitawapa tukio la Mama ameuawa na kuchinjwa vipande karibu 30, wa hapahapa Temeke Mbagala na aliyefanya na nitawaeleza alifanyaje”

“Nitawapa matukio ya Watu wameenda kwa Waganga wa kienyeji, Mganga ameona wana hela akawanywesha sumu wakafa akaiba hela akawazika bila taarifa, leo mnapokuta kuna matukio Watu wanasema Polisi ndio wanateka, Vyombo vya Dola vinateka, kuna vitu mnakosa uelewa na kwasababu mnakuja kwa mihemko hamuwezi kujibiwa kistaarabu hata kidogo”

"Halafu kwa mashinikizo mnasema tunataka kuingia barabarani, lazima Serikali iseme, kama tunataka kujenga Taifa letu ni vizuri tujenge mijadala ya kuulizana maswali, kuna vitu vinafanyika kama sanaa kuna vingine kweli Watu wamefanya, ebu niwaulize Baba na Mama wamefunga mlango wamekwenda ndani kulala asubuhi unaambiwa uko ndani Watu wameuana hivi niambieni kwenye mazingira hayo Polisi wanahusikaje?

kwahiyo Polisi awaambie laleni Mimi nipo mlangoni mpaka kunakucha inawezekana jamani?, kwahiyo Mlinzi wa kwanza kwa kila jambo ni Mwananchi mwenyewe”

“Hata Mimi Mkuu wa Mkoa unaweza kukuta hapa nalindwa lakini hawa wanaonilinda nakuwa nao nyumbani?, kama Mimi nitaondoka kwangu na Mkuu wa Wilaya tunakwenda huko Mbagala kunywa pombe tukishakunywa pombe tunachukua Wake za Watu halafu nasema watatufanya nini, watatupiga makofi huko na watanichinja, kwahiyo ulinzi wa kwanza ni wewe mwenyewe Raia”

“Mtu unazaa Mtoto huelewi ameenda wapi kutoka asubuhi hadi jioni, inafika saa mbili ndio unasema mtafuteni Mtoto, hivi kweli Mtoto huyo alikaa kwenye tumbo lako au la jirani?”

Pia soma
- RC Chalamila: Matukio ya Mauaji na Utekaji Watoto yapo lakini siyo kama yanavyoripitiwa, mengi siyo ya kweli

Source: Ayo TV
Anachosema ni sahihi
Watu wajilinde usikubali kuchukuliwa kwa kushikwa mkono kwa kuambiwa sisi ni askari...
Watu pia waunge mkono wakusanyike wengi na kupiga kelele...
Watu watatu wachukue mtu mmoja kwenye kikundi cha watu 40 hakuna prukushani yoyote wala aliyechukua video
Kauli aliyotoa huyo RC wa huko Dsm Bw. Chalamila unaweza ukaichukulia kuwa ni kauli nyepesi Sana, lakini ukiichambua kwa kina Sana ni Kauli nzito Sana, hii ni kutokana na Mazingira halisi ya kiusalama ambayo ni tete Sana yaliyopo hivi Sasa hapa nchini. Hii kauli unaweza ukaiita kuwa ni Declaration of a full scale war between the Innocent Civilians against the Police/Tiss Officials who are allegedly to be involved in the activities of Abducting Civilians. Hiyo kauli yake ni ya hatari Sana kwa mustakabali mwema wa usalama wa watu na mali zao. Sina uhakika kuwa kabla ya huyo RC kutoa kauli hii hadharani alijaribu kutafakari kwanza juu ya mapokeo ya wananchi kuhusu hoja yake hiyo. I' not sure.
Kauli Kama hiyo ya huyo RC wa Dsm iliwahi kutolewa na baadhi ya Watawala wa nchini Afrika ya Kusini enzi za utawala wa ubaguzi wa rangi, hali iliyosababisha reaction mbaya Sana kutoka kwa raia wa nchi hiyo (hususani watu weusi) ambao nao waliamua kujibu mapigo kwa kuanzisha kampeni ya kujihami, kampeni hiyo ilikuwa kali na ya hatari zaidi ambayo waliyoiita kwa jina la 'We are Fighting Back,' Hiyo kampeni ndio iliyoilazimisha Utawala wa Makaburu enzi hizo kuamua kutoa tangazo la Hali ya Hatari (The State of Emergency) kwa nchi nzima, tangazo hilo lilidumu kwa miaka mingi Sana na kugharimu maisha ya Watu wengi Sana katika nchi hiyo.
Nafikiri watawala wetu waliopo hapa nchini wanapaswa wajifunze historia ya mambo kama haya kutoka kwa wenzetu katika nchi zingine ambako nao pia waliwahi kupitia hali Kama hii tunayopitia Sasa hivi hapa Tanzania.
 
Chalamila ameongea kwa ujumla tu ,sisi tunataka majibu ambayo ni specific.

Waliomteka Sativa ndiyo hao hao waliomteka SOKA....Sativa amemtambua kiongozi wa watekaji mbona mpaka sasa hajakamatwa? Waliomuua kibao ni rahisi sana kuwapata lakini mpaka sasa hakuna chochote kinachoendelea wakati yeye ndiyo mwenyekiti wa ulinzi na usalama ngazi ya mkoa mzima wa DAR.

Mauaji ya visasi ,wivu na vitu vinafyofanana na hivyo yakitokea lazima yajulikane ndani ya muda mfupi na watuhumiwa wanakamtwa na tunawaona ila ukiona mauaji yametokea na hakuna aliyekamatwa basi jua ni "WASIOJULIKANA" wamefanya yao.......Sativa kashamtaja kiongozi wa "WASIOJULIKANA" RC ebu ruka naye ili tuone kweli upo serious.
 
Watu wataanza kujichukulia sheria mkononi, wananchi wanaweza wamuhisi mtu mtekaji wakamuua bila kuwa na ushahidi ….we CHIZI umeamrisha uvunjaji wa sheria bila hata kufikiri
 
Kwani polisi kazi yake ni nini?

Hivi anajitambua huyu kweli?
Mkuu, wasiojitambua ni sisi wananchi. Kauli kama hii ingetosha kuiondoa serikali madarakani, tena kwa wananchi kuvamia ikulu. Lakini wao wanajiamini kutoa kejeli kama hizi kwa sababu wanajua ''mi-tanzania'' ni mi-zoba isiyojitambua. Amini ninachokuambia. Bila sisi wananchi kujitambua hakuna kitu kitabadilika.
 
Chalamila ameongea kwa ujumla tu ,sisi tunataka majibu ambayo ni specific.

Waliomteka Sativa ndiyo hao hao waliomteka SOKA....Sativa amemtambua kiongozi wa watekaji mbona mpaka sasa hajakamatwa? Waliomuua kibao ni rahisi sana kuwapata lakini mpaka sasa hakuna chochote kinachoendelea wakati yeye ndiyo mwenyekiti wa ulinzi na usalama ngazi ya mkoa mzima wa DAR.

Mauaji ya visasi ,wivu na vitu vinafyofanana na hivyo yakitokea lazima yajulikane ndani ya muda mfupi na watuhumiwa wanakamtwa na tunawaona ila ukiona mauaji yametokea na hakuna aliyekamatwa basi jua ni "WASIOJULIKANA" wamefanya yao.......Sativa kashamtaja kiongozi wa "WASIOJULIKANA" RC ebu ruka naye ili tuone kweli upo serious.
Mkuu, hakutakuwa na majibu bila wananchi kuyataka na kuyadai kwa kutumia nguvu ya umma.
 
Back
Top Bottom