RC Chalamila awataka wakazi wa DSM wajilinde Wao na familia zao dhidi ya matukio hatarishi badala ya kuwatupia Polisi lawama

RC Chalamila awataka wakazi wa DSM wajilinde Wao na familia zao dhidi ya matukio hatarishi badala ya kuwatupia Polisi lawama

Anachosema ni sahihi
Watu wajilinde usikubali kuchukuliwa kwa kushikwa mkono kwa kuambiwa sisi ni askari...
Watu pia waunge mkono wakusanyike wengi na kupiga kelele...
Watu watatu wachukue mtu mmoja kwenye kikundi cha watu 40 hakuna prukushani yoyote wala aliyechukua video
watu watatu na smg unawazuiaje?
 
Mkuu wa mkoa wa DSM Albert Chalamila amewataka wananchi wa DSM kujilinda wao na familia zao dhidi ya matukio yoyote yanayoweza kuhatarisha Amani na Usalama wao

kwahiyo ulinzi wa kwanza ni wewe mwenyewe Raia”
Naunga mkono hoja ya RC Chalamila, tena nashauri kila kaya, kila familia ijengewe uwezo interms of capacity building, kila familia iweze kujilinda kama RC Chalamila alivyo jilinda kama alivyoeleza hapa This man is either a sadist or alimuua kibaka, akanywa bia kusherehekea?
View: https://youtu.be/DU2KYclh1l8?si=75ZpspiMj0XVDSbN
P
 
Kwa kauli hii CCM rasmi mmefungua milango ya kufanya uangalizi upya wa namna raia wanaweza pata mafunzo ya kujilinda bila kusahau kumiliki Silaha 😂
 
Mafwele weeh.
Msanii wa kuvamia na kupotea, kazi zako njema Sana machoni pa Mtawala wa Urithi toka nchi za Kisultani.
mawachukua misukule mnasingizia mambo mengineyo, si sawa.

acheni ramli chonganishi na ushirikina mara moja sawa gentleman na wenzako?🐒

ramli ndio satellites zenu sio?
 
Mkuu wa mkoa wa DSM Albert Chalamila amewataka wananchi wa DSM kujilinda wao na familia zao dhidi ya matukio yoyote yanayoweza kuhatarisha Amani na Usalama wao

RC Chalamila amesema SI HAKI kuwatupia lawama Polisi kwa kila Jambo.
---
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amewataka Wakazi wa Dar es salaam kutambua umuhimu wa kujilinda na kuzilinda Familia zao dhidi ya matukio yoyote yanayoweza kuhatarisha amani na usalama wao badala ya kuwatupia lawama Polisi kwa kila jambo.

RC Chalamila amesema hayo wakati akifanya ziara ya kukagua Zahanati ya Kurasini Wilayani Temeke leo September 27,2024 “Leo kwenye mkutano nitaongea baadhi ya vitu ambavyo Watu wanalalamikia utekaji sijui nini, leo kwenye mkutano nitawapa data namna Vijana wetu tuliowazaa wanavyoshiriki kwenye baadhi ya matukio, nitawapa tukio la Mama ameuawa na kuchinjwa vipande karibu 30, wa hapahapa Temeke Mbagala na aliyefanya na nitawaeleza alifanyaje”

“Nitawapa matukio ya Watu wameenda kwa Waganga wa kienyeji, Mganga ameona wana hela akawanywesha sumu wakafa akaiba hela akawazika bila taarifa, leo mnapokuta kuna matukio Watu wanasema Polisi ndio wanateka, Vyombo vya Dola vinateka, kuna vitu mnakosa uelewa na kwasababu mnakuja kwa mihemko hamuwezi kujibiwa kistaarabu hata kidogo”

"Halafu kwa mashinikizo mnasema tunataka kuingia barabarani, lazima Serikali iseme, kama tunataka kujenga Taifa letu ni vizuri tujenge mijadala ya kuulizana maswali, kuna vitu vinafanyika kama sanaa kuna vingine kweli Watu wamefanya, ebu niwaulize Baba na Mama wamefunga mlango wamekwenda ndani kulala asubuhi unaambiwa uko ndani Watu wameuana hivi niambieni kwenye mazingira hayo Polisi wanahusikaje?

kwahiyo Polisi awaambie laleni Mimi nipo mlangoni mpaka kunakucha inawezekana jamani?, kwahiyo Mlinzi wa kwanza kwa kila jambo ni Mwananchi mwenyewe”

“Hata Mimi Mkuu wa Mkoa unaweza kukuta hapa nalindwa lakini hawa wanaonilinda nakuwa nao nyumbani?, kama Mimi nitaondoka kwangu na Mkuu wa Wilaya tunakwenda huko Mbagala kunywa pombe tukishakunywa pombe tunachukua Wake za Watu halafu nasema watatufanya nini, watatupiga makofi huko na watanichinja, kwahiyo ulinzi wa kwanza ni wewe mwenyewe Raia”

“Mtu unazaa Mtoto huelewi ameenda wapi kutoka asubuhi hadi jioni, inafika saa mbili ndio unasema mtafuteni Mtoto, hivi kweli Mtoto huyo alikaa kwenye tumbo lako au la jirani?”

Pia soma
- RC Chalamila: Matukio ya Mauaji na Utekaji Watoto yapo lakini siyo kama yanavyoripitiwa, mengi siyo ya kweli

Source: Ayo TV
Ameongea vizuri tofauti na kichwa cha habari
 
Mnaweza kumlaumu ila kwa Mara ya kwanza ameongea point. Jukumu la usalama wetu ni letu wenyewe kuwa kuanzia halafu ndio hao vyombo vya kipolisi. Sema wangepunguza masharti kule kwenye umiliki wa silaha
 
Huyu naye ana akili kibaba!!

Hivi nani aliwahi kuwashutumu polisi kwa vifo vilivyotokea ndani ya nyumba za watu? Naona Dar tuna RC ambaye ama hazimtoshi kichwani au unafiki umemwondolea akili.

Polisi wanalalamikiwa kwa utekaji kwa sababu ni polisi waliwaita vituoni, halafu watu hao hawakurudi tena. Wengine baada ya kutekwa walipumzishwa ndani ya vituo vya polisi, kisha wakapotezwa. Wengine walichukuliwa mbele ya macho ya watu wengi, mbele ya polisi, watekaji wakajitambulisha kuwa ni polisi , wakiwa na smg na magari yasiyo na namba (ambayo huwa wanapenda kutumia agents wa serikali), halafu huyu punguani anakuja na mifano ya mambo yasiyoendana kabisa na matukio!! Hopless RC!!
Unafiki ndio tatzo
 
Naunga mkono hoja ya RC Chalamila, tena nashauri kila kaya, kila familia ijengewe uwezo interms of capacity building, kila familia iweze kujilinda kama RC Chalamila alivyo jilinda kama alivyoeleza hapa This man is either a sadist or alimuua kibaka, akanywa bia kusherehekea?
View: https://youtu.be/DU2KYclh1l8?si=75ZpspiMj0XVDSbN
P


Kauli aliyotoa huyo RC wa huko Dsm Bw. Chalamila unaweza ukaichukulia kuwa ni kauli nyepesi Sana, lakini ukiichambua kwa kina Sana ni Kauli nzito Sana, hii ni kutokana na Mazingira halisi ya kiusalama ambayo ni tete Sana yaliyopo hivi Sasa hapa nchini. Hii kauli unaweza ukaiita kuwa ni Declaration of a full scale war between the Innocent Civilians against the Police/Tiss Officials who are allegedly to be involved in the activities of Abducting Civilians. Hiyo kauli yake ni ya hatari Sana kwa mustakabali mwema wa usalama wa watu na mali zao. Sina uhakika kuwa kabla ya huyo RC kutoa kauli hii hadharani alijaribu kutafakari kwanza juu ya mapokeo ya wananchi kuhusu hoja yake hiyo. I' not sure.
Kauli Kama hiyo ya huyo RC wa Dsm iliwahi kutolewa na baadhi ya Watawala wa nchini Afrika ya Kusini enzi za utawala wa ubaguzi wa rangi, hali iliyosababisha reaction mbaya Sana kutoka kwa raia wa nchi hiyo (hususani watu weusi) ambao nao waliamua kujibu mapigo kwa kuanzisha kampeni ya kujihami, kampeni hiyo ilikuwa kali na ya hatari zaidi ambayo waliyoiita kwa jina la 'We are Fighting Back,' Hiyo kampeni ndio iliyoilazimisha Utawala wa Makaburu enzi hizo kuamua kutoa tangazo la Hali ya Hatari (The State of Emergency) kwa nchi nzima, tangazo hilo lilidumu kwa miaka mingi Sana na kugharimu maisha ya Watu wengi Sana katika nchi hiyo.
Nafikiri watawala wetu waliopo hapa nchini wanapaswa wajifunze historia ya mambo kama haya kutoka kwa wenzetu katika nchi zingine ambako nao pia waliwahi kupitia hali Kama hii tunayopitia Sasa hivi hapa Tanzania
 
Back
Top Bottom